Jerry Muro Mgeni rasmi Yanga VS TP Mazembe

Jerry Muro Mgeni rasmi Yanga VS TP Mazembe

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258


Mkuu wa kitengo cha habari cha klabu ya Yanga, Jerry Muro ndiye mgeni rasmi wa mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu, itapigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na tayari Yanga wametangaza mchezo huo ni bure, yaani mashabiki hawatalipa kiingilio.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza kuwa Muro ndiye atakuwa mgeni rasmi na kama kutakuwa na mgeni kutoka serikalini, Muro atabaki kuwa mgeni rasmi upande wa Yanga.

“Kweli hilo limepitishwa, Muro atakuwa mgeni rasmi,” kilieleza chanzo cha uhakika.

Juhudi za kumpata Muro kulizungumzia suala hilo, kuligonga mwamba kwa kuwa hakupokoea simu yake ya mkononi.
 
Yanga ilitakiwa kuwa na Afya kushinda TP Mazembe....nazingatia ki uchumi
walipaswa wawe na midege yao...na Kuwekeza kwenye Majengo yenye Afya na furaha .
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kazi kwelikweli.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mgeni wa mwendokasi
 
Back
Top Bottom