Jerry Muro unatia aibu

Unaonekana kabisa kuwa wewe ni shabiki wa Simba sc....!
 
Hivi Man United,Barca,R Madrid,Asernal,Milan na club kubwa Ulaya wana maofisa Habari?...
 
watu mna mahaba na soka haswaa.
 
Hyo Msumali ni shabiki mkubwa wa Simba toka.anasoma Kinondoni Muslim. Na sasa ni mmoja wa mwanachama wa kundi la Simba ukawa. Nauliza wapenzi wa Simba kule Shinyanga walimpiga kwa sababu gani?
 
Me cjui huyu jamaa kama taaluma yake ya uandishi haina weledi kabisaaa
 
Jery Muro na Nape hawana tofauti sana katika utendaji wao, wote wanaongozwa na mihemko yao binafsi kuliko taasisi inataka useme nini.
 
Hivi Man United,Barca,R Madrid,Asernal,Milan na club kubwa Ulaya wana maofisa Habari?...

Kwanini wakose? Wewe unafikiri hizi website zao wanaendesha akina nani. Hujawahi kuona TV zao? Mfano ni MUFC TV (Manchester United Football Club Television), Liverpool FC Tv nk..
Tofauti ni kwamba jinsi wanavyotoa habari ni tofauti na sisi.
 
Mkuu yanga hakuna ushilikina??

Unajichanganya!!!

1.Mtu anapohisi anarogwa japo mtu alishasema amliwafuata waandishi wa habari, huo ndio ushirikina
2.Mashabiki wa yanga wanapovamia gorini kutupa groves za gori keeper( rejea mapinduzi cup) huo ndio ushirikina
3.wale viongozi wa Yanga walifukua au kufukia vitu uwanjani mechi yao ya kwanza na Kagera Sugar, huo ndio ushirikina

Upoo!!!
 
hyo msumali ni shabiki mkubwa wa simba toka.anasoma kinondoni muslim. Na sasa ni mmoja wa mwanachama wa kundi la simba ukawa. Nauliza wapenzi wa simba kule shinyanga walimpiga kwa sababu gani?

mwehu wewe mi nilikwenda na timu kule nimejionea kila kitu,waliopiga ni wa stand united
 
PIA WACHEZAJI WA YANGA WAKOME KUGUSA KITAULO CHA IVO MAPUNDA,NA HUYU REFA ALIECHEZESHA MECHI YA MWISHO YA SIMBA NA YANGA NINA WASIWASI NAE,MANAKE AMEONYESHA WAZIWAZI ANAIMANI ZA UCHAWI,YEYE KAMA REFA KITAULO CHA IVO KINAmuhusu NINI ?
 
Unaonekana kabisa kuwa wewe ni shabiki wa Simba sc....!

TANGU ENZI ZA BABU YANGU ALIKUWAGA DAKTARI WA SIMBA MIAKA YA 60 na sisi wajukuu hutuambii kitu kuhusu simba,niko mombasa lakini naifuatilia club yangu vibaya sana
 
Kwanini wakose? Wewe unafikiri hizi website zao wanaendesha akina nani. Hujawahi kuona TV zao? Mfano ni MUFC TV (Manchester United Football Club Television), Liverpool FC Tv nk..
Tofauti ni kwamba jinsi wanavyotoa habari ni tofauti na sisi.

Hapo katika utoaji habari ndiyo kwenye tatizo...msemaji wa club anaropoka kupita maelezo,harafu anazungumzia masuala ya kiufundi,kitaabibu,mifumo ya uchezaji na mengineyo ambayo Hana utalaamu nayo...
 
Hapo katika utoaji habari ndiyo kwenye tatizo...msemaji wa club anaropoka kupita maelezo,harafu anazungumzia masuala ya kiufundi,kitaabibu,mifumo ya uchezaji na mengineyo ambayo Hana utalaamu nayo...

yeye fani yake ni rushwa tu,angalia tumashavu twake tulivonona!
 
Yanga haiamini katika Uchawi kama nyenzo ya kusaidia timu kufanya vizuri.....

Yanga ni lazima ikemee hayo mambo yanayodidimiza soka la tz kwa ujumla.

Tutakemea hadi muache kuamini huo ujinga.

Kitendo cha kuonyeshq kutokubali vitu kama hivi havimaanishi yanga ni wachawi.
 
yeye fani yake ni rushwa tu,angalia tumashavu twake tulivonona!

Hizo no Polojo tu........!

Hakuna kiumbe ambacho kinaishi Chini ya Jua sasa hivi Hakija jihusisha kwenye Rushwa ya namna moja ama nyingine.......#

Katika maisha yako ya kila siku .....kuna siku ,iwe kwa kujua au bila kujua ni lazima utoe au upokee takrima.
 
Huyo mwanachama wa simba alifanya kosa la mwaka kwenda kwenye jengo la kilabu ya yanga iwe kwa nia nzuri au mbaya. Kwa akili tu ya kawaida alipaswa kuelewa kuwa kitendo anachokifanya kilikuwa kinahatarisha maisha yake . Ni mwendawazimu tu anaweza kufanya hayo aliyoyafanya huyo mwanachama wa simba. Kwa upande mwingine huyo jerry muro hakutumia busara wala weledi kufanya hayo aliyoyafanya kwani ipo siku ataleta maafa. Ni wakati muafaka sasa kwa wakuu wake wa kazi au marafiki zake jerry muro wamweleze namna ya kufanya kazi wakati mwingine atumie tu "common sense" kwa mambo madogo madogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…