Jerry Muro unatia aibu

Jerry Muro unatia aibu

Beso

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Posts
216
Reaction score
59
kitendo chako cha kumlazimisha mwanachama wa simba aitwaye msumali aseme amekwenda kwenye klabu ya yanga kuroga ni kujidhalilisha wewe mwenyewe katika zama hizi bado unaabudu kurogwa mchana kweupe mbele ya mkutano wa waandishi wa habari.chanzo star tv habari saa mbili usiku huu.
 
Jamaa nimemshusha loooh hakuna kitu pale kumbe bichwa nyanya jamaa bado sana
 
waacheni wanayanga wenyewe ukiumwa na nyoka hata unyasi ................ !!!
 
Yaani tumemshangaa sana kupayuka kwa ujinga na kutia aibu sana eti anamlazimisha akubali ameenda kuloga,kifuu tundu yule jamaa
 
Hakika Simba Uchawi sasa unawatokea puani
 
Msumali anajulikana ni mchawi kupitiliza na hii si mara ya kwanza viongozi wa Simba Kukamatwa wakiwa wanaloga kwenye jengo la Yanga
 
Msumali anajulikana ni mchawi kupitiliza na hii si mara ya kwanza viongozi wa Simba Kukamatwa wakiwa wanaloga kwenye jengo la Yanga

ndugu zangu imani hizi za kishirikina hazitatusogeza mbele katika soka!tuamini katika uhalisia!
 
Mambo ya Yanga muwaachie Yanga,kwani si angaenda Kwenye Klabu yake ya Simba au kama aliambiwa waandishi wakitoka Jagwani wanaensa uwanjani Taifa basi agewafata uko Taifa.
 
Niliona hyo habari, nilitamani nizime TV maana anaongea upuuzi kama chizi. Anashindwa akili na kile kizee chao Akilimali.
 
ndugu zangu imani hizi za kishirikina hazitatusogeza mbele katika soka!tuamini katika uhalisia!

Ushauri mzuri kwa wanasimba.naamini wamekuelewa
 
maneno ya kiganga aliyokuwa anatambika jerry muro ndio yanasababisha soka letu haliendelei YANGA nao kila wakifungwa wanasingizia wamerogwa, TFF WAMCHUKULIE HATUA ILI IWE FUNDISHO KWA YANGA NZIMA , SABABU HATA MZEE AKILIMALI AMBAYE NI MKONGWE ZAIDI KATIKA KLABU YA YANGA HAKUTOA MATAPISHI KAMA ALIYOTOA HUYU KINUKA MKOJO KIBUZI KACHOKA JERRY MURO, ndo maana maduka ya wachaga yamejaa mazezeta. nina wasiwasi jinsi alivyopata hiyo nafasi
 
Huyu mtu anajisahau, moral authority anaitoa wapi wakati yeye ni mla Rushwa?
 
mla rushwa? ndo maana tumashavu twake tumenona mashaallah, wala hatushangai kwa picha aliyotoa jana tayar tumemjua yeye ni wa size gani
 
Sasa huyu shabiki wa simba alienda club ya Yanga kufanya nine?
 
Unasikitika nini yule kijana kupigwa......

Je umeajiliwa kwa madhumuni ya kukosoa wasemaji wa Yanga....?

Ni lazima imani za kishirikina zikemewe katika soka la tz..
Huwezi kukemea uchawi kwa kukaa kimya ..Hivyo alichofanya Jerry ni sahihi kabisa.

Kama unajisikia kuumia kama shabiki wa Simba sc kwa kuambiwa ukweli...basi no vyema uhamie Jangwani....mahala ambapo Ushirikina hauna nafasi wala haufumbiwi macho.
 
Haya matimu yenu ya yanga na Simba kuna wengine huwa tunaombea siku moja yashuke daraja.Hizo club hazijasaidia chochote kwenye soka la kibongo zaidi ya kusomeana masomo na hitima.Du aibu!.
 
Back
Top Bottom