Jerry Muro "Yanga kufa ni kufa "

Haya matokeo yalijulikana baada ya ile sare ya hapa nyumbani. Huyu Muro ananikumbusha msemaji wa serikali ya Sadaam ya iraq wakati ya vita na marekani miaka ya 90. Kila siku alikuwa akitangaza kuwa wanashinda tulipoona kimya tukamuona amekamarwa na wamarekani
 
Huyu msemaji wa vyura fc ajue waarabu hawanunuliki na wenye rekodi nzuri kwa waarabu ni simba tu hivyo aache kuropoka Sana.
 
Mbona bado tuko kimataifa au hufatilii mambo,Azam anarudi sisi tunacover ile nafasi yake na tutasonga kwenda hatua ya makundi.yanga bado ipo ipo sana kimataifa kama hupendi kula ndimu.
Yaah bado tunakwea pipa.
 
Huyu msemaji wa vyura fc ajue waarabu hawanunuliki na wenye rekodi nzuri kwa waarabu ni simba tu hivyo aache kuropoka Sana.

Naomba matokeo ya mwisho Simba ilipoenda kucheza Misri matokeo yalikuwaje?
 
Soka la bongo bhana, linachekesha sana, mi siichukii yanga kuiwakilisha nchi kimaraifa, lkn tumekuwa ni watu wa kisindikiza kila mwaka, hatuna mikakati endelevu kwa timu zote za tz, uwekezaji ni mgum lkn pia unahitaji maalifa zaidi, hii ni kero mf. baada ya mehi ya awal Yanga alikuwa na % ndogo sana za kushinda, vilabu vyetu kuna matatizo mengi sana
 
Utasemaje Yanga kafa wakati bado yuko kwenye mashindano ya kimataifa?Labda wewe mtoa mada ndio akili yako imekufa
 
Haitafika popote. Fanya yako ndugu. Labda kama ni kombe la vigodoro.
Ni ushauri mzuri, Ni kupoteza Muda kushabikia hizo timu maneno, sijasikia timu zinazochukua makombe wakijiita majina ya wakimataifa, ila sisi washirika tuna tambo kipita kiasi. Tukitolewa tunasema tumejitahidi, maana tulienda tukiwa Na uhakika wa kushindwa, shabashi soka la bongo.
 
Hatimae yametimia Yanga yatupwa nje mashindano ya Klabu bingwa Afrika.Kuna jamaa kasema eti Yanga kafa kiume napenda kumwambia Jerry Muro kuwa Yanga Kufa ni Kufa hakuna kiume wala kike
yanga oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Simba na Yanga kumbe zenyewe kwenye mashindano ya kimataifa ni Kama zilivyo Toto, na kagera sukari, zenyewe zinafurahia kushiriki na sio kwenda kushindana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…