Jerry Silaa atoa siku 100 kwa waliovamia maeneo ya wazi kuondoka Mara Moja

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Ngoja tuone maana umekuja na matamko mengi sana.

-
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa, amewataka waliovamia maeneo ya wazi kuanza kuondoka mara moja huku akiwaelekeza viongozi na watendaji wa wizara hiyo, wenye mamlaka ya kusimamia sheria kuhakikisha ndani ya siku 100 maeneo hayo yanakuwa wazi.

Silaa ameyasema hayo wakati akizumgumza na Menejimenti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mara baada ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, Dkt. Angeline Mabula, ambapo pia amewataka watendaji kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi ndani ya siku 100.
 
Huyu atanuka Sasa hivi. Hivi hajui kuwa waliovamia maneno ya wazi ni hao hao waliopendekeza ateuliwe na kupewa huo uwaziri?

Ndugu jamaa na marafiki wa familia ya yule rafiki yake aliyempigia debe mpk kupewa uwaziri ndiyo wanaongoza kwa kupora maeneo ya wazi. Narudia tena, Jerry Slaa atanuka Sasa hivi.
 
Kati ya viumbe watakaotaka kuosha jina ni huyu slaa, alitamani sana ubunge, lengo afike hapo alipo sasa (uwaziri)...

Bado hamjamjua vizuri mbunge wangu huyu... Namjua tangu akiwa Meya wa ilala, na nje(maisha yake binafsi nje ya Siasa)

Jerry huyu huyu ...!

Bado sinema ndio kwanza inaanza!....

Vuta kiti ukae swahiba ... Maana yajayo..... Yanafurahisha.
 
Ngoja tuone maana umekuja na matamko mengi sana.

-
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa, amewataka waliovamia maeneo ya wazi kuanza kuondoka mara moja huku akiwaelekeza viongozi na watendaji wa wizara hiyo, wenye mamlaka ya kusimamia sheria kuhakikisha ndani ya siku 100 maeneo hayo yanakuwa wazi.

Silaa ameyasema hayo wakati akizumgumza na Menejimenti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mara baada ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, Dkt. Angeline Mabula, ambapo pia amewataka watendaji kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi ndani ya siku 100.
Ukishaona kauli aina hizi ujue anaenda kuwa kiongozi fisadi kuliko wote
 
Hivi mnajua ya kwamba hii ni Moja ya wizara 8 zenye umate umate(fweza) ukiiacha zile zilizoko Frontline!?

Uzuri wa hii wizara Huwa haitolewi macho saana (haimulikwi)

Ila hela iko huku! Na hela nzuri ni ile inayo patikana kwenye eneo ambalo watu hawalitolei macho sana, kama hii wizara.
 
Ngoja tuone maana umekuja na matamko mengi sana.

-
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa, amewataka waliovamia maeneo ya wazi kuanza kuondoka mara moja huku akiwaelekeza viongozi na watendaji wa wizara hiyo, wenye mamlaka ya kusimamia sheria kuhakikisha ndani ya siku 100 maeneo hayo yanakuwa wazi.

Silaa ameyasema hayo wakati akizumgumza na Menejimenti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mara baada ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, Dkt. Angeline Mabula, ambapo pia amewataka watendaji kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi ndani ya siku 100.
Aanze na fuel filling stations zote zilizoibuka ghafla kwenye road reserves katika mji wa Dar hasa along Morogoro road baada tuu ya JPM kuondoka Duniani.
 
Kama wana akili Wakiyarudisha yawe maeneo ya mapumziko na jogging 🏃‍♂️
Yaani kuna majitu yenye kadi yamejigawiwa mpaka maeneo ya polisi
Shame on you guys
Watu hayo maeneo wameshajenga majumba wengine wameshusha maghorofa kabisa wanarudishaje kwa mfano?
 
Ngoja tuone maana umekuja na matamko mengi sana.

-
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa, amewataka waliovamia maeneo ya wazi kuanza kuondoka mara moja huku akiwaelekeza viongozi na watendaji wa wizara hiyo, wenye mamlaka ya kusimamia sheria kuhakikisha ndani ya siku 100 maeneo hayo yanakuwa wazi.

Silaa ameyasema hayo wakati akizumgumza na Menejimenti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mara baada ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, Dkt. Angeline Mabula, ambapo pia amewataka watendaji kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi ndani ya siku 100.
Kwahiyo ina maana ile Petrol station yangu niivunje au...?
 
Utatuzi wa migogoro ya ardhi unataka hekima na busara ya Hali ya juu sana kama alivyokuwa nayo William Lukuvi. Mtu yupo tayari kufa Kwa ajili ya kutetea kiapnde kidogo Cha ardhi yake. Jerry bado hajawa na uzoefu mkubwa lakini kapewa wizara nyeti ya ardhi, anahitaji kuwasikiliza wahanga kabla ya kutoa matamko.
Kwenye maadhimisho ya Nane Nane Mbeya Rais Samia akimjibu Bashe juu ya wanaodaiwa wavamizi wa ardhi ya Taasisi ya kilimo Uyole alimwambia alishughulikie Kwa kukaa mezani na wahusika bila kuleta taharuki Kwa Wananchi. Hii ndiyo busara na hekima iinayotakiwa. Wananchi wa Sae Mbeya wameyatumia maeneo miaka mingi toka mababu zao, wamepanda miti ambayo ina umri kuliko mheshimiwa Slaa, Taasisi ya Uyole ikatengeneza hati kinyemela bila kuwalipa fidia wamiliki wa asili. Itakuwa ni ukatili kuwabomolea wakazi nyumba zao. Ndiyo maana Kwa hekima mheshimiwa Lukuvi alitamka Taasisi ya kilimo warejeshe hati Kwa Wananchi kipande hicho Cha ekari 67. Lakini mheshimiwa Bashe anawasemelea mbele ya Rais kwamba ni wavamizi na wakaidi. Mheshimiwa Slaa karibu Mbeya utakutana pia na hili.
 
Huyu atanuka Sasa hivi. Hivi hajui kuwa waliovamia maneno ya wazi ni hao hao waliopendekeza ateuliwe na kupewa huo uwaziri?

Ndugu jamaa na marafiki wa familia ya yule rafiki yake aliyempigia debe mpk kupewa uwaziri ndiyo wanaongoza kwa kupora maeneo ya wazi. Narudia tena, Jerry Slaa atanuka Sasa hivi.
Ohooo ! Lakini kwa vyovyote vile wavamizi watakuwa ni watu wazito wenzie !
Ngoja tuone hii movie !
 
Mimi wakishaweza kuipima nchi nzima ili kuepusha ujenzi holela na slums itakuwa hoja yangu imejibiwa kwa kishindo.
 
Kuna vituo vingi vya mafuta vimejengwa maeneo ya wazi. Sasa wakivibomoa si mafuta yatakuuguza mwenyewe mhe. waziri. Au sijaeleweka.
 
Watu hayo maeneo wameshajenga majumba wengine wameshusha maghorofa kabisa wanarudishaje kwa mfano?
Kama waligawiwa kwa njia zisizo rasmi na hawana Hati miliki basi zitarudi tu kama sheria zipo
Ila kama na yeye atafungiwa Bahasha sawa
 
Back
Top Bottom