BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,767
- 23,198
kwa hiyo anachojaribu kusema sheria ya 2007 haifanyi kazi au?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sisi wapiga kura wake tumeisha listukia kitambo hivyo tunajipanga jinsi ya kumpiga chini huyu Zumbu kuku,ofosi ya kata ndiyo ameikimbia kabisa amepiga kambi mjini ili afanye madili yake tulimpigia kura ili asaidie kuboresha maendeleo ya jimbo kata yetu lakini amekimbia ameamishia ofisi yake Manispaa, hivi sheria inasemaje juu ya kuunganika ofisi ya meya na watendaji wa manispaa maana huyu kijana anapata maslahi yote ya watumishi Kuanzia chai,magazeti,usafiri ,gharama za masomo mpaka ulinzi wa nyumbani mfano mdogo ameenda Arusha kusoma Ada yake ni Shilingi za Kitanzania Milioni Sabini hivi ni kozi gani hapa nchini tena short course kwa gharama yote hiyo?bwana mdogo zuzu sana,anaharibu sifa ya vijana kushika hatamu kwa kuendekeza ujinga badala ya kufanya kazi.Watu tunakaa kwenye foleni zaidi ya masaa 3 lakini hilo halioni? .....natamani avuliwe gamba mapema kabla halijakomaa
Pasco sheria ya road reserve inaenda kinyume na by-laws za Halmashauri?
By-laws za halmaishauri ndizo zinazotakiwa kubadilishwa kuendana na sheria husika na kwa hivyo hizo ndo zibadilishwe ziendane na sheria.
Sisi wapiga kura wake tumeisha listukia kitambo hivyo tunajipanga jinsi ya kumpiga chini huyu Zumbu kuku,ofosi ya kata ndiyo ameikimbia kabisa amepiga kambi mjini ili afanye madili yake tulimpigia kura ili asaidie kuboresha maendeleo ya jimbo kata yetu lakini amekimbia ameamishia ofisi yake Manispaa, hivi sheria inasemaje juu ya kuunganika ofisi ya meya na watendaji wa manispaa maana huyu kijana anapata maslahi yote ya watumishi Kuanzia chai,magazeti,usafiri ,gharama za masomo mpaka ulinzi wa nyumbani mfano mdogo ameenda Arusha kusoma Ada yake ni Shilingi za Kitanzania Milioni Sabini hivi ni kozi gani hapa nchini tena short course kwa gharama yote hiyo? Mgambo wa Manispaa wapo, lakini analindwa na KK Security kwa gharama ya mlinzi mmoja shilingi milioni moja Kweli huu si ufisadi? hayo mabango anayopigia kelele ana mkono wake ,Tenda zote za Halmashauri ameshika yeye na Jamaa zake Uzuri ni kwamba sasahivi tuko macho sana kila hatua anayopiga tunayo na tunaendelea kukusanya ushahidi tatizo lake anaye mtegemea hana hata sauti katika nchi hii zaidi ya kufanya mbwembwe tu (RIZ 1).CAG Upo? TAKUKURU mpo? kazi kwenu nchi inaisha hivyo!!!!!!!!!!!!!!!
Hapo uko sahihi mkuu lakini na hili la uholela wa Jiji ni la muhimu sana makampuni yote makubwa yamehamishia ofisi zao Kinondoni ambako angalau sehemu nyingi zinafikika City Centre wanakimbia foleni na misongamano isiyo maana wamebaki machinga tu na wenye ofisi za mfukoni kama muheshimiwa Jerry!maana biashara zao ndiyo zinaendana na misongamano.ambazo hazina tija maana hata kodi zao hazieleweki wanalipia wapi?(kama huyu kijana anazimeki kila siku lakini hakuna anako lipa kodi) anaye bisha na tuanze kutoa vielelezo !Naona Tuanze na huu Mradi wa Vitofali ndio Ufisadi Usiosaidia Jiji kwa sasa (Pedestrian pavements kwa city center)
hana heshima huyu kijana, anatumia jazba nyingi kujibu suala ambalo liko wazi. atuambie kama ananufaika na hayo mabango.
hivi huyu kijana kwa mhe magufuli si kasisimizi aukuhusu Magufuli kufata sheria yuko sahihi ila na yeye anatakiwa afanye kazi yake sasa hivi mjini ni kuchafu kupindukia,msongamanoi wa watu,pikipiki na magari pamoja na hivyo vyombo kuegeshwa katika mabarabara
tumechoka na maneno yao tunataka wafanye kazi
Wajameni huyu meya huyu namfahamu, kiukweli ni kati ya hazina kubwa chache za vichwa vya ukweli CCM ilivyonavyo japo nakiri kwenye suala hili ameshindwa kujieleza vyema.
Sehemu yuko right na sehemu yuko wrong na Magufuli yuko right kwa asilimia 100%.
Ni kweli Halmashauri zina mamlaka yake ambayo hayapaswi kuingiliwa na serikali kuu ikiwemo mabunge yake (mabaraza ya madiwani) ambayo yanamamlaka ya kisheria kujitungia bylaws zake. Hivyo mabango yapo kisheria na yana mikataba halali na halmashauri husika, hivyo meya yuko right, mabango hayo hayawezi kungolewa kwa agizo la siku 7 kama Magufuli alivyogiza!.
Alichofanya Magufuli ni kusisitiza matakwa ya kisheria ya utekelezaji wa sheria mpya ya road reserve ya mwaka 2007 ambayo inakwenda kinyume cha by laws za halmashauri, hivyo licha ya sheria hiyo kupitishwa, halmashauri zilipaswa kutengua bylaws zake na kuzioanisha na sheria hiyo mpya, kitu ambacho hakikufanyika na badala yake Halmashauri zimeendelea kurenew mikataba ya mabango kwa sheria za zamani ili kuendelea kuvuna pesa nene!.
Hata hivyo ukweli wa mambo, uinguliaji mkubwa wa road reserve sio mabango, ni vibanda vya biashara na wafanya biashara ndogondogo ambao hawako covered kwenye by laws za halmashauri.
Alichotakiwa kusema huyu meya ni kuamuru utekelezaji wa kuwaondoa hao wafanya biashara kwanza na kusema mchakato wa kuyaondoa mabango ufuate matwakwa ya kisheria ili halmashauri zisiingie kwenye migogoro ya kisheria na kesi za madai kufidia hasara ya kuvunja mabango ya watu yaliyokuwepo kabla ya sheria hiyo kupitishwa!.
Mji wa Dar es Salaam ni kama mji wa Mbuzi; kila mahali ni choo, kila mahali ni hotel, kila mahari ni sehemu ya biashara, kila mahari ni parking, kila mahari kuna gereji, n.k. Bahati mbaya huu ndo mji mkuu wa kibiashara wa nchi hii. Gharama tunayoliingiza taifa hili, kutokana na uzembe huu wa kupanga mji mkuu, ni kubwa mno kuliko hivyo vifedha mbuzi vya matangazo wanavyopata Manispaa. Meya hajaangalia msitu anaangalia mti.
Kuhusu by-laws za manispaa. Mimi si mwanasheria, ila najua kuwa katika nchi kuna Katiba, Sheria, na vi-sheria (ndo hizi by laws). Kwa kawaida ikiwepo sheria ambayo inapingana na katiba inatakiwa ibadirishwe ili iendane na matakwa ya katiba vinginevyo sheria hiyo inakuwa si halali. Vile vile hizi by-laws inatakiwa ziwe zinabadirishwa ili kuendana na sheria mama za nchi. Zisipobadirishwa zinakuwa sheria mfu na kuendelea kuzitumia ni uzumbukuku.
Kama sheria ya bara bara imetungwa mwaka 2007, kwa nini hadi leo manispaa hawajarekebisha by-laws zao kuendana na sheria mama? Au ndo tunaanza kutengeneza vi-falme ndani ya nchi? Na kwa nini meya anapuliza vuvuzela kwa nguvu hivyo wakati yaliyozungumzwa ni maamuzi ya serikali kuu? Naamini hapa kuna tatizo.
Hali ni mbaya sana kwa huu mji wa Dar na kadri siku zinavyoenda hali inazidi kuwa mbaya. Upangaji wa mji haupo na mambo yanafanyika kiholela. Na wanaosababisha upangaji holela ni hawa wanaojiita serikali za mitaa sababu ya ubabaishaji mkubwa uliojaa huko. Hatuwezi kuendelea hivi hivi hadi milele.
Kuweka kumbukumbu sawa tu !
HakunA mtu simpendi kama Jerry Slaa ! Namchukia tu