Pre GE2025 Jerry Silaa tunakuhitaji Ukonga kwa sababu zifuatazo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Smart Gin hizo akili yako inaharibika unasema nn ukienda kuongea huo ujinga kivule na makofi utapigwa Kama anakununulia pombe kunywa Ila acha kuropoka....
Bishana kwa hoja mkuu
 
Hili ndio tatizo la wanasiasa wengi wa Bongo walioferi wanadhani kuwanywesha Pombe wapumbavu kama huyu na kuwanunulia smartphone za promotion ndio wanasolve tatizo, kumbe ndio wanazidisha hasira watu.

Nina nyumba Italian Kigenzi nimehama Kule Kwa sababu ya barabara, thread za kula kulala kama huyu wacha tu nikae kimya, watu wa Ukonga wanajuwa cha kumfanya akithubutu kugombea tena.
 
Kama tunaishi Industrial waambie Serikali waje wabomoe. Sifa za Jerry usihusishe na Ukonga. Labda ana sifa zake unazozijua wewe tena za Kipuuzi tu. Ni Waziri wa Ardhi tunamkaribisha aje abomoe
 
Mungu atupe uhai 2025 siyo mbali, ila ilikuwaje ukanunua sehemu haina barabara? Lawama kwa mbunge hapo zinakujaje? Kwa nini hukuenda kununua mitaa ambayo ina lami tayari narudia 75% ya ukonga haikuwa mahsusi kwa ajili ya makazi ya watu ndiyo maana huku kesi za uvamizi haziishi..unataka uwekewe barabara eneo la uvamizi? Au miye ndio sielewi
 
Kama tunaishi Industrial waambie Serikali waje wabomoe. Sifa za Jerry usihusishe na Ukonga. Labda ana sifa zake unazozijua wewe tena za Kipuuzi tu. Ni Waziri wa Ardhi tunamkaribisha aje abomoe
Miye labda sijui, jukumu la mbunge ni kutengeneza barabara? Au ni jukumu la tarura? Barabara zinatengenezwa kwa fungu lipi? Labda tuanzie hapo kabla ya kuanza lawama ..binafsi naishi viwege kwa mpemba mwaka wa 13 sasa kabla ya hapo nilikuwa naishi mzambarauni kwa miaka 10 na ni muathirika mzuri tu wa hizi barabara huwa inanilazimu kupanga chumba mjini ili niwahi kibaruani lakini sijawahi kuona kosa la mbunge kwani huku nilihamia mwenyewe kwa utashi wangu...na nilipokuja kugundua haya maeneo mengi ni ya uvamizi huwa naomba tu Mungu huruma ya serikali kwa wananchi wake lakini mbunge hahusiki na lawama zozote
 
Mkipewaga misaada na viongozi mtulie, sio kutia hasira watu.
Mxxxiiiiieeeew
Nenda kaishi mbezi kuna lami kila mtaa...huwezi ukaja sehemu ukaanzisha mji kisha unamlaumu mbunge on a personal capacity kwani yeye ndiye alikwambia uhamie huko....
Mkipewaga misaada na viongozi mtulie, sio kutia hasira watu.
Mxxxiiiiieeeew
 
Njaa mbaya sana
Njoo na hoja chief, ubovu wa barabara za mtaa ni suala la halmashauri la sehemu husika bora hata mara Mia lawama zingeelekezwa kwa diwani maana yeye huwa anapata fungu la maendeleo sasa mbunge kweli yaani unazungumzia mbunge...Jerry kama Jerry akili nyingi mtateseka sana
 
Ubovu wa barabara wakulamiwa ni madiwani katika halmashauti yako mzee mbunge hahusiki familiarise yourself with position descriptions za hawa watu kwanza
Hakuna kitu kibaya kama kukwepa respobilities, nashangaa inapokua ni negative issues kila MTU hataki kuwa accountable. Mbona Taifa Stars wakishinda games huwa mnapongeza Samia na sio kocha (ni mfano)! Leo barabara zikiwa mbovu ni za madiwani, zikiwa nzuri ni za Samia. Sawa jumapili njema
 
Jerry pesa za mfuko wa jimbo huwa unazipeleka wapi? Maana hata madiwani wako wenyewe hawakuelewi
 
Huwa siquote post za kula kulala na wapumbavu kama wewe, Leo umebahatika Tu.

Uliza Kata ya Buyuni kwenye Jimbo la Ukonga uambiwe mpuuzi mkubwa wewe, mradi wa viwanja vya serikali upo Buyuni, na nyumba za Pspf zipo Buyuni.

JF iongeze vigezo vya kuruhusu watu wa kupost kwenye jukwaa la siasa, thread ipitiwe Kwanza na moderator kabla ya kuruhusu kupublish pumba kwenye forum.
 
Matusi ya nini? Nyumba za pspf buyuni zinahusiana nini na hii post naomba TP namba ya project ya buyuni ambayo nadhani ni ya mwaka 2005 nikuonyeshe jinsi wavamizi mlivyo haribu mipango miji, kama huna nikusaidie ambapo kwa kifupi tu ni ile kesi ya hekari elfu tatu kati ya mwalimu Mbambo na wazee saba wakiwemo kina matangula yaani mmenunua maeneo mmeuziwa na wakurya mmenda kung'oa mawe kisha unakuja kutukana watu humu
 
Labda kwa haraka haraka nikusaidie maeneo ya uvamizi, yenye kesi au hukumu imeshatoka tayari ukitoka pugu sekondari baada ya kupita reli mkononwa kushoto kama unaelekea viwege yale maeneo yana mgogoro kitamboo na hukumu ishatoka tayari ikifika njia nne mbondole kama unaelekea ofisi za serikali ya mtaa hukumu imetoka na waliovunjiwa walivunjiwa ving'ang'anizi walibaki kuna eneo linaitwa uvikiuta pia greda lilipita ila kuna wabishi bado wapo ambao ndiyo wanakuja na matusi humu kudaibwanataka barabara ukifika mbondole kuna kesi kubwa ambayo imezimwa kisiasa kwa kuwataka wamiliki wa sasa walipe fidia ila kiukweli hii kesi itaibuka muda siyo mrefu kwani mh Lukuvi alipokuwa waziri wa ardhi alimaliza kwa hekima zake hapantunazungumzia kaya elfu tatu...binafsi nina mchoro wa kutoka ardhi wa maeneo yote haya ambapo unakuta jitu limejenga kwenye let say pb (public building) halafu ndiye wa kwanza kutukana viongozi eti anataka barabara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…