PostGE2025 Jerry Silaa Waziri pekee aliyeshindwa kutetea Jimbo, Bakari Shingo mbunge mteule wa jimbo la Ukonga

PostGE2025 Jerry Silaa Waziri pekee aliyeshindwa kutetea Jimbo, Bakari Shingo mbunge mteule wa jimbo la Ukonga

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
1762324646325.png
Katika jambo ambalo halikutarajiwa katika jimbo la Ukonga na wachunguzi wengi na watafiti wa siasa ni kitendo cha Mhe.Jerry William Silaa na aliyekuwa Waziri wa Habari Teknolojia na Mawasiliano ya Habari kushindwa kutetea jimbo lake mbele ya Bakari Shingo, aliyekuwa mgombea ubunge wa Act katika jimbo la Ukonga ambaye sasa ni mbunge mteule wa jimbo hilo

Silaa anakuwa waziri pekee aliyeangushwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 katika hatua za kura inayoshirikisha wananchi wote wa Tanzania wenye sifa za kupiga kura

Kwa maana hiyo Bakari Shingo anakuwa miongoni mwa wabunge 4 wa Tanzania bara walioshinda kupitia tiketi ya chama cha Act Wazalendo ambapo kimepata majimbo 4 Tanzania bara ambayo ni Ukonga, Nkasi kaskazini, Tunduru kusini, na Kigoma Kaskazini.

1762324471339.png

Bakari Shingo mbunge mteule jimbo la Ukonga
Act Wazalendo​
 
Hayo ni maigizo ya CCM tu, hakuna uchaguzi uliofanyika.
 
Ndiyo kusema G55 na kujipendekeza kote kule wamenyimwa hata jimbo moja! Au watazawadiwa viti maalum vichache vya kwenda kuwakuna akina nani wale... vitambi kule Dodoma!

Mambo ya aibu sana haya!
 
Nkasi Kaskazini 👐👐👐👐

2010 - 2020 - Ally Kessy (CCM)
2020-2025 - Aida Khenan (Chadema)
2025-2025+ - ACT Wazalendo

Chadema hawakushiriki, Aida Khenan hajahama chama chake.

Angekuwepo bila shaka angetetea jimbo lake.
 
Ndiyo kusema G55 na kujipendekeza kote kule wamenyimwa hata jimbo moja! Au watazawadiwa viti maalum vichache vya kwenda kuwakuna akina nani wale... vitambi kule Dodoma!

Mambo ya aibu sana haya!

Mwaka huu hakuna viti maalumu kwa Upinzan.

Katiba inasema ni lazima Chama kinachopeleka viti maalumu Bungeni kupata 5% ya kura halali kwenye uchaguzi mkuu.

Naiona Safar ya Kisiasa za Ushindan kwa Zitto inaishia hapa.

Zaid zaid atapewa ukuu wa Mkoa/wilaya akatulie.(alishasema Mama Amemuahidi atamfanyia kitu)

Na ACT tutegemee Viongozi wapya.

Kwakuwa Bakar Shingo bila shaka ni Ustadhi ni vyema Akapewa wadhifa ndan ya ACT maana atakubalika na ACT wa Znz pia...
 
Back
Top Bottom