Jerry Slaa Kumbuka waonee huruma wananchi wa Sae Mbeya

Jerry Slaa Kumbuka waonee huruma wananchi wa Sae Mbeya

Mpap Ndabhit

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
331
Reaction score
416
Leo alfajiri Tarehe 13/4/2024 limepita gari la matangazo katika jiji la Mbeya na vitongoji vyake kwamba waziri wa ardhi atakuwa ukumbi wa mkapa kusikiliza na kutatua KERO.

Slaa unajua uamuzi wako uliotofautina na WA mtangulizi wako Lukuvi unavyowatesa wananchi wanaotakiwa kubomolewa makazi Yao na kilimo Uyole!

Slaa unajua wanajeshi wanawabughuzi wananchi wa Sae Katika makazi Yao Huku hao wanajeshi wakiendelea na ujenzi katika eneo Hilo lenye mgogoro!

Unajua ushauri mzuri wa chama Cha mapinduzi aliotoa mwenezi Makonda juu ya utatuzi wa mgogoro huo haujayekelezwa hata Moja!

SASA Ni KERO Gani unazosikiliza na kutatua?
 
Watu wanatengeneza Perdiem bhana.

Hakuna cha kusikiliza kero wala nini.
 
Ongezea nyama kwenye uzi mkuus

Unajua suala hili huyu mheshimiwa wetu analifahamu sana Kwa kuwa alilikuta likiwa limeshatatuliwa na mheshimiwa Lukuvi. Wananchi wameruhusiwa kujenga na wamejenga kweli. Ajabu akaja na mambo mapya akisikiliza upande mmoja wa mgogoro na wananchi kuonekana wavamizi kwenye ardhi Yao.
Clip IPO ya Lukuvi, IPO ya Makonda wameliaddress vizuri jambo hili.
Wananchi wamebaki wanalia kilio Cha samaki.
Mheshimiwa aje amalize mgogoro huu!
 
Wadau mimi naomba kuuliza, hili swala la waziri kwenda kusikiliza kero, kiutendaji limekaa sawa kweli?
Nikiangalia kuna mipango na sera nyingi sana ndani ya wizara ya ardhi ambazo zilianzishwa na sielewi zilipoishia, sasa najiuliza waziri anapata wapi kuda wa kwenda kutatua kero moja moja?
Ukiangalia sasa hivi kuna tatizo sugu la ukataji na uuzwaji holela wa viwanja..

Kulikuwa na program ya upimaji wa maeneo ambayo yalikuwa hayajapangwa, sijui hiyo program imeishia wapi
Kulikuwa kuna program ya urasimishaji wa makazi holela,sijui ilifia wapi
Kulikuwa kuna program ya kutengeneza masterplan mpya ya mikoa na majiji sijui imefia wap. Nk nk nk

Waziri anapata wapi muda wa kuzurura huku mitaani? waliopo chini yake wana kazi gani?
 
Binafsi naona ni vizuri sana mawaziri kwenda mtaani kuwasikiliza wananchi na kutatua KERO ambazo zimekaa kiutawala zaidi. Kuna baadhi ya mambo yanahitaji tamko la waziri au kiongozi wa kisekta. Wana Sae Mbeya waziri Lukuvi alitatua mgogoro wa zaidi ya miaka 50 Sasa akaja Silaa akaufufua mgogoro Kwa kwenda kinyume na Lukuvi. Aidha alimsikiliza Bashe Kwa pamoja wakampotosha mheshimiwa Rais na hivyo kupeleka kilio Kwa wananchi wa eneo Hilo. Ni uonevu na ubabe mkubwa wawatawala dhidi ya watawaliwa.
 
Back
Top Bottom