Mpap Ndabhit
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 331
- 416
NakaziaOngezea nyama kwenye uzi mkuu
Ongezea nyama kwenye uzi mkuus
Clip IPO ya Lukuvi, IPO ya Makonda wameliaddress vizuri jambo hili.Unajua suala hili huyu mheshimiwa wetu analifahamu sana Kwa kuwa alilikuta likiwa limeshatatuliwa na mheshimiwa Lukuvi. Wananchi wameruhusiwa kujenga na wamejenga kweli. Ajabu akaja na mambo mapya akisikiliza upande mmoja wa mgogoro na wananchi kuonekana wavamizi kwenye ardhi Yao.
Binafsi naona ni vizuri sana mawaziri kwenda mtaani kuwasikiliza wananchi na kutatua KERO ambazo zimekaa kiutawala zaidi. Kuna baadhi ya mambo yanahitaji tamko la waziri au kiongozi wa kisekta. Wana Sae Mbeya waziri Lukuvi alitatua mgogoro wa zaidi ya miaka 50 Sasa akaja Silaa akaufufua mgogoro Kwa kwenda kinyume na Lukuvi. Aidha alimsikiliza Bashe Kwa pamoja wakampotosha mheshimiwa Rais na hivyo kupeleka kilio Kwa wananchi wa eneo Hilo. Ni uonevu na ubabe mkubwa wawatawala dhidi ya watawaliwa.Wadau mimi naomba kuuliza, hili swala la waziri kwenda kusikiliza kero, kiutendaji limekaa sawa kweli?
Nikiangalia kuna mipango na sera nyingi sana ndani ya wizara ya ardhi ambazo zilianzishwa na sielewi zilipoishia, sasa najiuliza waziri anapata wapi kuda wa kwenda kutatua kero moja moja?
Ukiangalia sasa hivi kuna tatizo sugu la ukataji na uuzwaji holela wa viwanja..
Kulikuwa na program ya upimaji wa maeneo ambayo yalikuwa hayajapangwa, sijui hiyo program imeishia wapi
Kulikuwa kuna program ya urasimishaji wa makazi holela,sijui ilifia wapi
Kulikuwa kuna program ya kutengeneza masterplan mpya ya mikoa na majiji sijui imefia wap. Nk nk nk
Waziri anapata wapi muda wa kuzurura huku mitaani? waliopo chini yake wana kazi gani?