Jerusalem: Shambulio la risasi kwenye basi lajeruhi watu 8

Jerusalem: Shambulio la risasi kwenye basi lajeruhi watu 8

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Watu wanane wamejeruhiwa vibaya baada ya mtu mmoja mwenye silaha kuvamia basi moja mjini Jerusalem na kuanza kufyatua ovyo risasi.

Miongoni mwa watu walio athirika na shambulio hilo ni mwanamke mjamzito ambaye amelazimishwa kujifungua mapema chini ya uangalizi wa madaktari baada ya kuwa na hali mbaya.

Kupitia andiko lao kwenye mtandao wa Twitter, wizara ya mambo ya nje ya Israeli imelaani vikali kitendo hiki “Tunawaombea majeruhi wapone haraka. Shambulio hili kwenye mji mkuu wa Israel, mji mtakatifu kwa dini zote tatu ni jambo linalopaswa kulaaniwa vikali”

Shambulio hili limetokea mapema siku ya jumapili, August 14, 2022 wakati basi moja likiwa limepaki likisubiri abiria wapande.

Chanzo: Abc News
 
Kumbe Mossad ni mkwara tu hamna kitu. Yani matukio kama hayo yanatokea kiwepesi katika nchi inayosemekana ina intelejensi kali. Wanatafuna tu misaada ya wamarekani kijinga jinga. Hapo jumba bovu watawaangushia binamu zao wapalestina.
 
Back
Top Bottom