Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Yapo Mambo yanafanywa na wagombea wa Chama cha Mapinduzi wakiwemo vijana yanatia najisi jamii wanayotaka kuiongoza. Jery Slaa kumnawisha mwanamke miguu kama njia ya kuomba kura ni fedhea na ulaghai usiokubalika.
Siasa ni hoja, tunategemea kuwa na viongozi wajenga hoja siyo viongozi wanafiki wanaofanya mambo ambayo wakichagulia hawatayafanya tena. Nchi haina tatizo la waosha miguu, ina tatizo la miundombinu, nchi haina tatizo la wapembua mchele ina tatizo la huduma za afya, nchi haina tatizo la watoa burudani ina changamoto kubwa ya maji na elimu. Tunataka watu wakutuletea haya, tunataka watatua changamoto siyo waosha miguu.
Acheni kujidhalilisha na kujidhalilisha chama, mnakifanya chama kionekane cha kisanii kwa sababu mnayofanya kwenye kampeni siyo realistic.
Mimi siwezi kupiga kura kwa mwanaume anayejidhalilisha na kukaa saloon kisa Ubunge kwa sababu hiki anachokifanya ndicho atakachokifanya akifika Bungeni, atalala na kujenga hoja zisizolitoa taifa hapa lilipo.
Wanawake wa CHADEMA katika majimbo yote nchini wanaonyesha ujasiri na moyo mkuu kuliko matendo yanayofanywa na hawa wanaume wasiojitambua. Inakera sana kuteua wagombea wa aina ya Jerry.