Jesca Magufuli achangia Ujenzi Nyumba ya Katibu UVCCM Wilaya ya Chato. Asisitiza Kumuenzi Hayati Magufuli

Jesca Magufuli achangia Ujenzi Nyumba ya Katibu UVCCM Wilaya ya Chato. Asisitiza Kumuenzi Hayati Magufuli

Huyu ndio Jesca aisee!🤔🥺 Kuna sehemu niliwah kutana nae tukaongea kwa muda mrefu kidogo sikumbuki hata kama nilimuuliza hata jina mpaka namuona kwenye picha hapa ndio nikakumbuka anyways ukikutana nae nivigumu sana ku notice ndio Jesca wa hayati JPM nilichopenda kutoka kwake hakuonesha majivuno yoyote Yuko low key sana
 
Nani huyo? Magufuli alifukuza Watoto Wetu Udom wale special Diplomakwa madai ni vilaza wakati Watoto wake walipa 0.

Zambi itamtafuna huko aliko.
nina mdogo wangu wa damu alikuwa hapo aisee vijana walipewa masaa 24 wasionekane hapo! Kama huna nauli, unatokea mkoa wa mbali utajijua mwenyewe, magari ya washawasha yakawa yanarandaranda. Dogo alifika tabora usiku wa manane
 
"Mimi nikasema si vibaya nikajumuika na vijana wenzangu (UVCCM) Wilaya ya Chato katika ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Chato na kuhakikisha inakamilika, nikasema nichangie kidogo nilichobarikiwa kuhakikisha kazi za Chama na pia siyo mwisho, nitaendelea kuchangia zaidi na zaidi mpaka kuhakikisha nyumba imekamilika kabisa" - Jesca Magufuli (Mtoto wa Hayati JPM)

Jesca Magufuli amesema kuwa amewiwa kujitolea baadhi ya vifaa ujenzi vya nyumba ya Katibu wa UVCCM kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za vijana wa CCM ambao wameonyesha dira ya uwajibikaji

Bi. Jesca Mafuguli ametoa vigae kwa ajili ya kukamilisha nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Chato ambayo kwa sasa imefikia Asilimia 90 ya ujenzi huku akiwaasa vijana kuendelea kushirikiana katika Kulijenga Taifa la Tanzania kupitia serikali ya awamu ya Sita.

Naye, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka UVCCM mkoa wa Geita, Rubein Saganyika Amewataka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Chato kumuenzi Rais wa awamu ya tano, Hayati Dk John Magufuli kwa kuchapa kazi na kuiishi slogan yake ya Hapa Kazi Tu.

Aidha, Ruben Sagayika amewaomba vijana kuendelea kujitolea kwa ajili ya kukijenga chama ambapo amemushukuru binti wa Hayati Dk Magufuli ambaye ni Jesca Magufuli kwa kujitolea baadhi ya vifaa ujenzi kukamilisha ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM Chato.

View attachment 2937331View attachment 2937332View attachment 2937333View attachment 2937335View attachment 2937336
Ni vizuri, japo jesca anasubiri uteuzi kabla sa100 hajamalizia kipindi hiki.
 
Back
Top Bottom