Ndugu zangu Watanzania,
Kuna watu wana nyota zao ,kuna watu wana bahati zao,kuna watu wana vibali vyao,kuna watu wana Sehemu zao kwenye Mioyo ya watu,kuna watu wana mvuto wao,kuna watu Hawatumii nguvu kupenya na kuteka mioyo ya watu.
Saa chache baada ya kupita tangia Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga kupost Picha akiwa na Mtoto wa Hayati Daktari Mwalimu John Pombe Joseph Magufuli, Ndugu Jesca John Magufuli Imekuwa ni Gumzo Nchini Kenya.
Kwani wakenya Wameonyesha kukoshwa sana na picha hiyo ,wameonyesha kuvutiwa sana na muonekano wa Binti huyo Mrembo wa asili mwenye staha ,adabu,heshima, unyenyekevu,ukarimu na upendo wa hali ya juu sana.
Imefikia hatua wakenya kutamani Binti Huyo Mbichi mithili ya Bamia Teta apewe nafasi ya kuwahutubia Wakenya hususani vijana ili waweze kupata chakula cha ubongo yaani maarifa. Hasa kwa kuzingatia ametoka katika Nchi ambayo licha ya kuwa na makabila zaidi ya 120 lakini watu wanaishi kwa upendo ,umoja na mshikamano pasipo ubaguzi wa aina yoyote ile. Na kwamba mtu yeyote yule anaweza kuwa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa bila kujali kabila lake au dini yake au jinsia yake au kipato chake.
Wekenya wengine wamefikia hatua ya kusema kuwa Binti huyo anapaswa kushawishiwa ili achukue Fomu ya kugombea Ubunge katika uchaguzi Mkuu wa hapo Baadaye Mwishoni Mwa Mwaka huu.
Hata Mimi nimewaunga mkono wa Kenya kuwa Huyu Binti anastahili kuingia Bungeni ,Maana hata vijana tu wa Huko Chato na Geita kwa ujumla wake wamekuwa wakikoshwa na kuvutiwa sana na ukaribu ambao amekuwa nao kwa jumuiya ya vijana . Kwa kuwasaidia katika mambo mbalimbali kama ambavyo miezi michache iliyopita aligawa bure kabisa Pikipiki mkoa mzima wa Geita. Na kuwaacha vijana wakitabasamu na kufurahi.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.