Jeshi la Akiba Tanzania (Mgambo) watumike kwa Ulinzi kwenye maeneo ya Umma

Jeshi la Akiba Tanzania (Mgambo) watumike kwa Ulinzi kwenye maeneo ya Umma

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !

Salaam kwako Mtanzania; wewe ni mwema sana.

Ninaombi ambalo limekaa kama pendekezo; Naomba kuuliza Je, ni kwanini hawa wataalamu wa Ulinzi ambao ni Jeshi la Akiba wasitumike moja kwa moja kwenye maeneo ya Umma kama sehemu ya kutoa huduma ya Ulinzi na kuimarisha Usalama kwa wananchi.

(Napenda kukiri yakuwa sina utaalamu wala ujuzi wowote juu ya Usalama na ulinzi; naomba litambulike na kuchukuliwa kama wazo tu)

Mfano, Maeneo ya makazi ya Raia, maeneo ya Biashara, Mashuleni, Hospital, Vyuoni.

Kuhusu namna ya malipo ya Posho kwa hii huduma tunaweza kukubaliana kama taifa kupitia ninyi viongozi kuwatengea Bajeti maalumu na ipitie Jeshi la Wananchi Tanzania.

Faida
1. Tutachochea Uwekezaji na ukuaji wa Biashara hapa nchini - sababu kuu kuimalika kwa Usalama.

2. Ajira kuwa kubwa kwa ngazi zote na maeneo yote.

3. Kupunguza matukio ya viashiria vya ugaidi na kuboresha huduma ya ulinzi wa kutosha.

4. Biashara zitafanyika masaa 24 kwa siku 7 miaka yote maana tutakuwa na amani nyakati zote.

5. Tutaliongezea thamani sana Jeshi letu hili la Akiba Tanzania.

Asante.
 
Wakati zamani ilikuwa kuwa mgambo ni kudharaulika, eti leo hii imekuwa kuwa mgambo yenyewe ni dili mpaka uhonge ndio unakuwa mgambo....
 
Hiyo ni kazi ya polisi kama wameshindwa kazi watuambie

Nikuulize leo hii; hawa askari wa akiba wanafanya kazi gani?

Mbona huwa wanatumika kwenye Usimamizi wa mitihani ya kitaifa au uchaguzi, je Jeshi la Polisi huwa wapo wapi?
 
Back
Top Bottom