Jeshi la Iran lazima jaribio la USA kuiba mafuta ya Iran

Jeshi la Iran lazima jaribio la USA kuiba mafuta ya Iran

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Hizi habari niliziona mtandaoni nikahisi labda si kweli ila imethibitisha kimataifa, hii ni aibu mno kwa marekani hawa jamaa ni majambazi hivi kumbe

Kikosi cha IRGC cha Iran chazima uharamia wa jeshi la Marekani katika Bahari ya Oman

Nov 03, 2021 11:25 UTC

[https://media]

Operesheni makinii na iliyochukiwa wakati mwafaka na wanajeshi shupavu wa kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) imefanikiwa kuzima jaribio la uharamia na wizi wa mafuta uliosimamiwa na manuwari ya kijeshi ya Marekani katika maji ya Bahari ya Oman.

Televisheni ya al Alam imeripoti kuwa, mashujaa wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wamezima jaribio la operesheni ya manuwari ya jeshi la Marekani iliyojaribu kuiba mafuta yaliyokuwa yamepakiwa katika meli ya mafuta ya Iran.

Manuwari hiyo ya jeshi la Marekani ilipora na kuchukua meli iliyokuwa imesheheni mafuta ya Iran katika Bahari ya Oman na kupakua mafuta yake na kisha kuyapakia katika meli nyingine na kuielekeza kusikojulikana.

Hata hivyo, kikosi cha anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kilitekeleza operesheni kinzani na kushusha wapiganaji wa kikosi hicho juu ya meli hiyo na kuitwaa na baadaye kuilekeza kwenye maji ya Iran.

Jeshi la Marekani viliifuata meli hiyo kwa kutumia helikopta na meli kadhaa za kivita, lakini limeshindwa kutokana na kuingia nguvu kubwa zaidi ya vikosi vya IRGC.

Baada ya hapo, jeshi la Marekani liliifuata meli hiyo ya mafuta kwa kutumia helikopta kadhaa na meli za kivita, lakini jaribio hili pia lilishindwa kutokana na azma kubwa ya la Walinzi wa Mapinduzi.

Jitihada kubwa za askari wa Marekani za kujaribu kusimamisha na kuzuia meli hiyo zimefeli na kwa sasa shehena ya mafuta iiliyokuwa imeporwa na askari wa Marekani iko katika maji ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

4by719641b21821ytl8_800C450.jpg
 
Hamna kitu hapo ni fix hizo za hao wenye imani kali.
 
Ila ww udini utakuua maskini, mdini kupindukia ww. You won't get ahead with such a caliber! Ww una ubaguzi mkubwa sana wa kidini. Character mbovu sana hiyo, kwa mentality hiyo ufukara utakupiga vibaya sana
 
hakuna kitu kama hicho, Kuna sheria za kimataifa zinambana US, na taasisi za kimataifa hazijalala kama unavyolala wewe
 
Ila ww udini utakuua maskini, mdini kupindukia ww. You won't get ahead with such a caliber..!! Ww una ubaguzi mkubwa sana wa kidini. Character mbovu sana hiyo, kwa mentality hiyo ufukara utakupiga vibaya sana
Udini umeingiaje hapo? Yeye kakleta taarifa, labda udini unao ww
 
hakuna kitu kama hicho, Kuna sheria za kimataifa zinambana US, na taasisi za kimataifa hazijalala kama unavyolala wewe
Kwahio mkuu huamini kamaarekani ni wizi wa mafuta na wakitaka kuiba mafuta but wameshtukiwa na kupewa onyo wakasepa
 
No country in past 3 to 4 decades ago has humiliated the terrorists (US) like the might republic of Iran.
 
Kwani wizi wameanza leo?
Hawa na marafiki zake wa West wote ni maharamia wakubwa

Iraq wameiingiza kwenye mgogoro ili waibe mafuta na mwisho wakaiba na artefacts zote waliiba na zililetwa London, New York na Paris

Dhahabu nyingi sana waaliiba wanajeshi wa Marekani
Haya sio kuwa nimeyasoma tu bali nilikuwepo Iraq miaka hiyo

Mafuta mengi walikuwa wanaiba kupitia Syria mpaka Uturuki
Tulikuwa tunapishana na malori ya mafuta yakisindilizwa na wanajeshi hao
 
Back
Top Bottom