Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Kupitia ukurasa rasmi wa account ya Jeshi la Israel (IDF) kupitia mtandao wa Facebook. Jeshi la Israel limeshutumu kundi la Hamas kutumia Raia kama ngao ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Israel.
Intelijensia ya Israel inasema kuwa imefanya utafiti kujua makombora ya Hamas yanatoka upande gani, na wamegundua Makombora yanayorushwa na Hamas, yanarushwa kutoka maeneo ambayo ni Kambi za watu.
Hivyo kuwawia vigumu Israel kurudisha mashambulizi hayo, kukwepa kuwalipua raia ambao miongoni mwao kuna hao magaidi ya kundi la Hamas. Radar ya Israel imesoma makombora ya Hamas yanarushwa kutoka Mahospitalini, Mashuleni, Misikitini, Mihahawani, maeneo ya kidiplomasia ambayo kimsingi ndiko raia wameenda kujihifadhi.
Jeshi hilo limesema Hamas hawana huruma kwa raia wagaza kwa sababu wanawaweka raia kwenye hatari ya kushambuliwa na Israel, Hamas wangekuwa na nia nzuri basi wasinge hatarisha maisha ya raia, ila wako radhi kuwatumia raia kama ngao hili kufa nao.
Isingekuwa Raia kutumiwa kama ngao, Jeshi la Israel lingekuwa lishafyekelea mbali kikundi chote cha Hamas. Lakini bado Jeshi la Israel linawalazimu kutumia Wanajeshi wa ardhini kufika maeneo hayo yenye watu hili kuwadhibiti magaidi. Israel imepania kutowaacha salama wafuasi wa kikundi cha HAMAS, na imeahidi kuwafuta kwenye uso wa Dunia.