Jeshi la Israel laua Wapalestina 10 huko Ukingo wa Magharibi

Jeshi la Israel laua Wapalestina 10 huko Ukingo wa Magharibi

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Vikosi vya Israel vimewauwa Wapalestina tisa, wakiwemo watatu waliojihami kwa silaha, raia watatu, na kuwajeruhi wengine zaidi ya 90, katika Ukingo wa Magharibi.

Watu walioshuhudia na madaktari wamesema kuwa mauaji hayo yamefanyika katika operesheni iliyoendeshwa kwenye eneo tete, lenye kukaliwa kimabavu la Ukingo wa Magharibi.

Kwa upande wake jeshi la Israel limethibitisha kufanya operesheni zake katika mji wa Nablus, lakini halikutoa taarifa zaidi kuhusu maafa yaliyotokea.

Vyanzo kutoka upande wa Palestina vinasema makamanda wawili wa kundi linalojiita Islamic Jihad waliuawa pamoja na mtu mwingine aliyekuwa kajihami kwa silaha.

Neblus na mji wa karibu wa Jenin inalengwa na operesheni za kijeshi, ambazo zimekuwa zikiongezeka kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, tangu yalipotokea mashambulizi ya Wapalestina.

Wizara ya Afya wa Palestina inasema kwa mwaka huu pekee Wapalestina 57, wakiwemo wenye kujihami kwa silaha pamoja na raia, wameauwa.
 
Attachments

  • 64787131_1005.jpg
    64787131_1005.jpg
    82 KB · Views: 4
HILI JESHI NI BORA SANA, ONA LINAVYOPAMBANA NA JESHI GUMU LA PALESTINA.HAkIKA IDF NI SHIDA.Hawaogopi hata manati.
Jeshi la wapalestina ambao hawana uwezo WA kumiliki au kutengeneza silaha nzitonzito amka tumia Akili usiwe kama wale wanaosema Israel ni Taifa takatifu wakati hata hawamjui yesu our saviour.
 
Jeshi la wapalestina ambao hawana uwezo WA kumiliki au kutengeneza silaha nzitonzito amka tumia Akili usiwe kama wale wanaosema Israel ni Taifa takatifu wakati hata hawamjui yesu our saviour.
Unaumia ukiwa wap mkuu.
 
Jeshi la wapalestina ambao hawana uwezo WA kumiliki au kutengeneza silaha nzitonzito amka tumia Akili usiwe kama wale wanaosema Israel ni Taifa takatifu wakati hata hawamjui yesu our saviour.
Ungetulia kidogo tu ungejua nimemaanisha nini.
 
Back
Top Bottom