Jeshi la Polisi Dodoma linamwogopa Dogo Manda? Kuna nini nyuma ya Pazia?

Jeshi la Polisi Dodoma linamwogopa Dogo Manda? Kuna nini nyuma ya Pazia?

Nasema Uongo Ndugu Zangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
279
Reaction score
779
Miaka kama 20 iliyopita katika kijiji cha Chigongwe nje kidogo ya manispaa ya Dodoma, yalitokea mauaji ya mlinzi aliyekuwa akilinda yard ya kampuni ya Konoike kipindi kampuni hiyo inatengeneza barabara ya Dodoma - Singida - Mwanza. Inasemekana mlinzi huyo alipigwa mshale na watu waliodhaniwa kuwa wezi waliokuja kuiba mafuta. Jeshi la polisi lilimtia mbaroni mwananchi mmoja wa kijiji hicho aliyefahamika kwa jina la Dogo Manda na aliendelea kushikiliwa kwa miaka kadhaa kisha akaachiwa huru akarudi kuendelea na maisha yake kijijini hapo.

Mwaka 2020, mfanyabiashara mmoja wa kijiji cha Chigongwe maarufu kwa jina la Jairosi akiwa nyumbani kwake ambapo pia katika eneo lake ameweka miradi mbalimbali kama kuuza vinywaji, duka la mahitaji mbalimbali ya nyumbani, mashine ya kusaga nafaka nk akiwa katika biashara yake, mwanaume mmoja alikuja na kusalimia watu, kisha aliuliza mahali alipo Jairosi, akaoneshwa na watu waliokuwa pale, kwakuwa mzee Jairos alikuwa anawahudumia wateja wa vinywaji, mtu huyo alienda pia akajifanya kama mteja wa bia, baada ya dakika chache alichomoa bastola na kuanza kumimina risasi kwa Jairos, mzee akajitahidi kukimbia ila hakuweza kufika mlangoni akaanguka, yule jamaa akaondoka, wateja walio kuwepo pale kila mmoja alitafuta namna ya kunusuru uhai wake.

Baada ya hali kutulia, wananchi walimchukua na kumpeleka zahanati lakini alikata roho, polisi walikaa kimya mpaka mke wa marehemu alipoenda kulalamika ngazi za juu ndipo wakaja kuchukua maelezo na wakatokomea.

Mwaka jana kijana mmoja anayefanya shughuli za bodaboda na kuuza mchanga kijijini hapo Chigongwe, akiwa nyumbani kwake, usiku wa manane, alisikia sauti ikimwita nje, alitaka kumfahamu aliyekuwa akimwita, yule bwana akajitambulisha na kijana akaifahamu sauti yake na alikuwa ni rafiki yake wa kijiji jirani ambaye alidai kuwa anaomba hifadhi kwa usiku mmoja, kijana wa watu akatoka akafungua mlango, ghafla akanyooshewa mtutu wa bunduki, kwakuwa hakuwa na option nyingine, kijana aliamua kujaribu kujinusuru kwa kumrukia ghafla na kumkata mtama, kwakuwa yule jamaa hakutegemea alijikuta ameanguka chini na bunduki yake, kijana akamrukia nawakaanza purukushani pale chini huku kijana akiomba msaada.

Mama yake mzazi alikuwa mtu wakwanza kutoka maana anaishi hapo hapo na mama alipotoka chakwanza alishika mkanda wa ile silaha kuhakikisha jamaa hawezi kuitumia, pia alichomoa simu ya mhalifu na kuitupa kando, mara watu wengine wakaja na jamaa akajikuta matatani maana wananchi walianza kumtembezea kichapo, walitokea watu wenye busara wakaomba asipigwe bali atoe maelezo, wakati huo polisi nao waliwasili ila wananchi walitaka ajieleze kwanza ndo achukuliwe na polisi.

Kijana akaeleza kuwa ametumwa na mtu anayeitwa Dogo Manda, na akaenda mbali zaidi kwa kusema hata Jairos aliuwawa na yeye kwa maelekezo toka kwa Dogo Manda kwasababu ya wivu wa kibiashara, wakati mahojiano yakiendelea, ile simu ikaanza kuita (ile ya mhalifu) na askari wakaipokea na kuweka loud speaker, aliyekuwa akipiga ni Dogo Manda na baada ya askari kupokea aliuliza mbona unachelewa, umesha maliza kazi, polisi mmoja akauliza kazi gani? Dogo Manda baada ya kubaini ni sauti ngeni, akakata simu.

Yule kijana akaeleza mahali alipoitoa ile silaha, na mahali ambapo kuna mtu anawatengenezea silaha (polisi waliokuwepo wanajua) baada ya hapo polisi waliondoka naye, mke wa Jaios alivyopata habari hizi akaenda polisi kufuatilia kinacho fuata maana mhalifu yule alieleza kuwa yeye pia alihusika kwenye mauaji ya mume wake na alitumwa na Dogo Manda, polisi kuona hivyo, wakaja kumkamata Dogo Manda, baada ya siku chache wakasema yule mhalifu amefariki kwa kipigo cha wananchi, hivyo baada ya miezi kama 4, wakamwachia huru Dogo Manda, kwakuwa bado wananchi walikuwa na hasira naye, aliamua kutokomea kusiko julikana na baada ya miezi kadhaa akarudi, akafungua biashara nyingine katika eneo la Nala baada ya biashara za Chigongwe kusuasua.

Jeshi la polisi mkoani Dodoma, kuweni makini sana, mambo mengine mnalea wenyewe, ngoja niishie hapa lakini mmetengeneza picha mbaya sana...
 
Nashindwa kuelewa jamaa ni kitengo??kama ni kitengo mbona mauaji yake sio ya kimkakati? Nawashauri wananchi wa eneo husika waende maeneo ya farkwa, gonga au kwamtoro kwa wasandawe wakamuajiri mlenga shabaha wa mshale aje hapo amalize kazi!!kama polisi wameshindwa basi wananchi watumie sheria jamii!!!huo ni ujinga na na uzembe!!!
 
Nashindwa kuelewa jamaa ni kitengo??kama ni kitengo mbona mauaji yake sio ya kimkakati??Nawashauri wananchi wa eneo husika waende maeneo ya farkwa,gonga au kwamtoro kwa wasandawe wakamuajiri mlenga shabaha wa mshale aje hapo amalize kazi!!kama polisi wameshindwa basi wananchi watumie sheria jamii!!!huo ni ujinga na na uzembe!!!
Angekuwa kitengo si wangefanya hata utaratibu wa kumhamisha, maana watu wana hasira naye sema wanashindwa kumwanza.
 
Back
Top Bottom