Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi Tanzania limesema limepokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari na wananchi wakitaka kufahamu hali ya usalama nchini, na limethibitisha kuwa hali ya usalama inaendelea kuwa shwari.
"Tumepokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari na wananchi wakiulizia hali ya usalama hadi sasa ikoje. Jeshi la polisi Tanzania lingependa kuwafahamisha Watanzania na wageni waliopo nchini kuwa hali ya usalama nchini ni shwari. Pamoja na kwamba leo tarehe 7 7 2026 ni sikuukuu ya Saba Saba na watu wako kwenye mapumziko lakini wengine wanaendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii.
Tunaendelea kuwahakikishia wananchi kwamba kwa ushirikiano na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tutaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wakati wote. Tunaendelea kutoa wito kwa wananchi tuendelee kutumia mitandao ya kijamii vizuri na kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa kuandaa na kusambaza taarifa za uongo, unganishi, kujenga chuki na kuzisambaza.
Soma Pia: Polisi Dodoma: Tumeweka askari wa kutosha sana Mtaani, hali hiyo itaendelea mpaka tutakapoona tarehe iliyopangwa tumepita kwa Usalama
Pia tujiepushe na kusambaza taarifa unazotumiwa kupitia mitandao ambazo hazijadhibitishwa na mamlaka husika. Kwani kwa kufanya hivyo kwa pamoja ni makosa ya jinai kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 16 na sheria nyingine za nchi. Aidha tujiepushe kuwa kila kitu kinachosambazwa kupitia mitandao ya kijamii ni sahihi. Badala yake pata taarifa sahihi kutoka mamlaka zinazohusika kutoa taarifa sahihi kama vile vyombo vya ulinzi na usalama."