hivi kweli unategemea dereva atasema kinyume na bosi wake ni kitu hakiwezekani, dereva wa mbowe hawezi kuwa shahidi wa kuaminika kwani lazima atapendelea basi wake.Vipi kuhusu dreva,,huyu ndo atatoa mwanga,maana kwa mujibu wa ripoti,mbowe alipiga kelele,dreva ndo mtu wa kwanza on scene,,hivyo itakuwa alikua hata hajaondoka pale.
Sasa ww ndiyo umeshindwa kuelewa, polisi wao wamesema kabisa eneo LA tukio na wakasema kabisa 'kulikuwa na watu' maana yake ni kwamba ushahidi waliouchukua ni wa 'watu' na 'makelele' tafsiri yake polisi wamesema specifically aina gani ya ushahidi ambao wao wameuzingatia ni wa kelele,watu, polisi wangekuwa wamesema wamechukua ushahidi wa CCTV wangesema express kabisa kwa hiyo huo ushahidi wa kielectroniki ambao ni admissible mahakamani wameuruka wameenda kwenye ushahidi wa kusikia,na ushahidi wa 2nd degree ambao ni secondary evidence badala ya primary evidenceUmesoma taarifa yote ya uchunguzi ukakuta CCTV cameras hazijahusika kukamilisha uchunguzi? Au ndo kusoma habari kwa mihemuko ya kisiasa..
Kama unajua kuchambua taarifa za kiitelinjesia utaelewa kuwa CCTV kamara zilitumika Ila Kama kichwa chako nikwa ajili ya kufugia nywele pekee utaendelea kuuliza CCTV camera mpaka Mh Mbowe na Joyce wanapata mtoto.
"Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa" Msemaji wa jeshi la polisi.
Hakuna mnafki anayeweza kudumu chadema,ni suala la muda tu!kwa fikra ambazo Ndio Kiwakilishi cha nafsi zako hazisomi Huru kiasi cha kujihisi ni mwanachadema kifikra,uanachadema hauwakilishwi na fikra kama zakoSisi Wanachadema tunamuachia chama bora tuende Nccr mageuzi tu
CDM ndio wanafiki wakubwa kwà kiwango Cha juu sana kabisa!! Msitufanye WaTZ wote ni mburura na mkaendelea kutafuta huruma zetu!!!Hakuna mnafki anayeweza kudumu chadema,ni suala la muda tu!kwa fikra ambazo Ndio Kiwakilishi cha nafsi zako hazisomi Huru kiasi cha kujihisi ni mwanachadema kifikra,uanachadema hauwakilishwi na fikra kama zako
Sikushangai maana logic ya nilichoandika hukielewi. Don't judge a book by its cover. Neno uliloona ni like lakini post nzima hujaelewa. Vijana wa ccm mbona madarasa ya MEMKWA bado yapo sio mkajiendeleze?Umepani
Hivi kuna mpumbavu zaidi yako!!
Yaani Like kwako Jambo Kubwa na lamana
Aliyeongea habari ya bei hapa ni nani?leta hoja siyo makurupukoCDM ndio wanafiki wakubwa kwà kiwango Cha juu sana kabisa!! Msitufanye WaTZ wote ni mburura na mkaendelea kutafuta huruma zetu!!!
HV kweli mamia Yote ya Wanachama waliohama kwenu ni kufikia Bei tu!? Na Hakuna Hata mmoja anaewaongelea mazuri wote Hawa wanawasingiza kisa wamefika Bei!? Huwez kudanganya watu wote muda wote Ila unaweza danganya watu wote kwà muda tu!!
Itawarudia wenyewe. Subiri.CHADEMA mko wapi mwenyekiti anazalilishwa
Tatizo ni uchaguzi. Watu wanahaha kukashifiana. Mwenye akili timamu apuuze haya yote ila mwenye akili pungufu ashililie bango.Taifa linaangamia kwa kusa watu wenye busara,
Taifa la uongo na umbeya,Chuki na Vsasi.
Nilishangazwa sana na Taarifa hii kuwa haina tofauti na ile iliyotolewa na Spika Job Ngungai.
Taarifa ya Kiupelelezi,imepitiabungeni kwanza, kisha ndio polisi wakaitowa rasmi?.
Sijui ndio mtindo mpya wa matukio ya jinai nchini?
Lkini lile tukio la Tundu lisu,naona jeshi la polisi halijatoa taarifa hadi leo,
Bali ni Bunge lililodai kuwa hawamjui alipo.
Na kwa hiyo alifutwa ubunge wake ,na huenda akirudi akakutana na kesi za kujibu mahakamani kwa kusingizia kupigwa risasi na kujeruhiwa, tukio ambalo polisi hawna habari nalo hadi leo.
Hii ndio Tanzania MPYA tuliyonayo.
Tanzania ni Taifa la ajabu sana.
Ikiwa Mbowe aliudanganya Umma anaweza kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria?
Lakini ,Muruto mwanzo alisema kuwa Polsi inazo taarifa za Mbowe kushambuliwa na watu kwa kukanyagwa bila ya kutumia silaha.
Leo imekuja nyingine kuwa hakuna kabisa tukiio la aina hii, bali ni uzushi,
Lakini Uchunguzi unaendelea.
KESHO TUTAPATA KUWA CAMERA ZINAONESHA NINI?
sheria hairuhusu mke wako kuwa shahidi wako ,dreva ameruhusiwahivi kweli unategemea dereva atasema kinyume na bosi wake ni kitu hakiwezekani, dereva wa mbowe hawezi kuwa shahidi wa kuaminika kwani lazima atapendelea basi wake.
ndio maaana ushahidi wa majirani ulikuwa wa muhimu sana kuliko hata derrva
Kumbe unaandika hata hujasoma wala kusikia taarifa ya Polisi?Lini mbowe alisema alipiga kelele sana?
Kuna aib gani kutaja chuo alichosoma mtu?Sio vizuri kukitaja.
Watu wenye uelewa mdogo wanaweza kudhania una kidhalilisha.Kuna aib gani kutaja chuo alichosoma mtu?
Utakuwa umelewa chakarii.Huoni support yangu imekuletea traffic?,uzi wako ulidoda bila boost ujumbe ungemfikia nani sasa?
Tulia kijana unafiki wenu tunauelewa kila mahali!! Kamwe hatuwezi ruhusu wahuni wachache watuletee maigizo hapaAliyeongea habari ya bei hapa ni nani?leta hoja siyo makurupuko
Sasa mamaangu kajaje hapa? Inawezekana ukawa mtoto sio rizki wewe! Maana ndio lugha zao hizi!Hongera kwa kuona like
Kitu kikubwa kwako
Ukipewa like
Unajihisi dunia ya mamako Eh!!
Huo ndio ukilaza wa Ufipa
Jeshi la Polisi Tz limejaa waliofeli shule, na vyeti feki
View attachment 1476358View attachment 1476359
USHAHIDI wa awali wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu madai ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe umeonesh kuwa siku hiyo ya tukio Mbowe alikuwa amelewa chakali na alizunguka kwenye kumbi mbalimbali za starehe zinazouza vileo ikiwemo ya Royal Village.
Pia ushahidi huo unaonesha mbali ya kuwa kwenye maeneo hayo ya starehe alikuwa nyumbani kwa mzazi mwenzake Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema na kwamba hata taarifa za kwamba ameshambuliwa zinatia shaka kwani mashahidi wote ambao wameojiwa hakuna anayethibitisha uwepo wa tukio hilo zaidi ya Mbowe mwenyewe na dereva wake.
Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi hilo David Misime amesema Juni 9 mwaka huu walitoa taarifa ya awali kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Mroto kuhusu tukio la lililoripotiwa kuwa Mbowe amelezwa jijini Dodoma kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa wakati anaingia nyumbani kwake .
Misime amesema baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ya awali wamekuwa wakipokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari wakitaka kufahamu matokeo ya uchunguzi kuhusu taarifa iliyofikishwa Kituo cha Polisi Kati Dodoma.
"Napenda kujulisha kuwa Jeshi la Polisi limeendelea kufanya upelelezi wa kina kuanzia kwa mhanga mwenyewe wa tukio ambaye alidai kuwa muda wa saa saba hivi usiku akiwa kwenye ngazi ya kuingia nyumbani kwake akiwa na anatoka kwa mzazi mwenzake aitwaye Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema anayeishi eneo la Medeli Mjini Ddoma alishambuliwa na kuumia kwenye mguu wa kulia.
"Mhanga wa tukio hilo alidai wakati anashambuliwa alipiga kelele nyingi kuomba msaada ambao aliupata kutoka kwa dereva wake ambaye naye alipiga simu kwa Joyce Nkya kisha hospitali iliyoko takribani umbali wa kilometa tano nje ya Jiji la Dodoma pasipo umuhimu wa kutoa taarifa Polisi kabla ya kwenda kwa Joyce Nkya na Hospitali,"amesema Misime.
Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa .
"Hata hivyo kwa mujibu wa wa mashahidi hawa hakuna hata mmoja aliyeweza kusikia kelele hizo au kuona mbowe akishambuliwa. Kwa mantikini hiyo ushahidi pekee unaozumngumzia kushambuliwa ni maelezo ya mhanga wa tukio(Mbowe) pamoja na dereva wake.
"Ambayo kwa hali ilivyo sasa yanatia shaka kuhusu ukweli wa tukio hili.Mashaka hayo yanaongezeka zaidi pale tulipobaini kuwa nyumbani kwa Mbowe alikuwepo kijana wake aitwaje James Mbowe ambaye hawakuona umuhimu wa kumjulisha kuhusu tukio lililotokea hapo nyumbani badala yake waliona umuhimu wa kumjulisha Jocye Nkya aliyekuwa mbali na eneo la tukio,"amesema.
Pia amesema uchunguzi wa Jeshi la Polisi nchini umethibitisha kuwa siku ya Juni 8 mwaka huu Mbowe alitembelea sehemu kadhaa za starehe zinazouza vileo ikiwepo ya Royal Village na kupata kinywaji.
"Hata hivyo alipofika hospitali alioneana akiwa katika hali ya ulevi chakari kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.Tunaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hili, hivyo tunaomba wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi huo wazilete kwetu. Tutaendelea kutoa taarifa kwenu kadri ushahidi utakavyopatikana,"amesema Misime kupitia taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari.
Pia soma
> News Alert: - Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana
> Freeman Mbowe na Joyce Mukya wamtumia Mjomba wa Mtoto kupata cheti cha kuzaliwa
> Mhe. Mbowe na Mhe. Joyce Mukya mtafanya hili suala kuwa siri mpaka lini?
> Joyce Mukya ni nani? Pamoja na kutokuwa active kwenye Siasa bado anapeta ubunge CHADEMA zaidi ya miaka 10