DCP. Zuberi chembera naibu mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai amefahamisha kuwa katika tukio hilo dereva wa gari aitwae msina sharif (29) mkaazi wa kidoti na msaidizi wake aitwae abdalla bakari sheha (28) mkaazi wa kidoti walipoteza maisha na watu wengine wawili walijeruhiwa ambao ni mohammed issa mohammed (10) mwanafunzi wa skuli ya msingi kidoti na hamza abdalla abasi (10) mwanafunzi wa skuli ya msingi kidoti, majeruhi hao walikuwa watembea kwa miguu wamegongwa wakati gari hilo limepoteza muelekeo na kugonga mti/mkungu, wamelazwa hospitali ya kivunge kwa matibabu.