LGE2024 Jeshi la Polisi laonya mikusanyiko isiyo halali Uchaguzi Serikali za Mitaa, lasema raia wasijichanganye na uvunjivu wa amani

LGE2024 Jeshi la Polisi laonya mikusanyiko isiyo halali Uchaguzi Serikali za Mitaa, lasema raia wasijichanganye na uvunjivu wa amani

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Justification ya kuzuia baadhi ya mikutano ya kisiasa na kampeni za vyama fulani ileee inawekwa kwenye mstari!


Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limevionya vyama vya siasa na kuvitaka kuepuka mikusanyiko isiyo halali katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Kupata nyuzi za kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Akizungumza na viongozi wa makundi mbalimbali yakiwemo siasa, dini, wazee pamoja na watu wenye ulemavu, Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa amesema jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha amani inatawala katika kipindi cha uchaguzi na kuonya mikusanyiko isiyo rasmi

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Taifa Jamal Babu amesema watahakikisha wanafuata maagizo ya kamanda Mutafungwa kwa kuhakikisha wanajiepusha na mikusanyiko isiyo rasmi.
 
Back
Top Bottom