Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,866
Reaction score
5,747
Ni baada ya Kamati ya Bunge iliyopewa kazi ya kufuatilia Sakata la Lugumi kuthibitisha kuwa vifaa mashine hizo zimefungwa katika vituo vyote.

Agizo hilo limetolewa na Bunge kupitia kwa Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson wakati akiahirisha Bunge la 11 leo mjini Dodoma
==========

Habari wakuu,

Leo akihitimisha bunge, naibu spika ametolea ufafanuzi utekelezaji wa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole(AFIS), hoja iliyojengwa kutokana na mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) kwa kutokamilika kwa mradi huo.

Agizo la bunge lilimtaka afisa masuhuli wa jeshi la polisi kuhakikisha mfumo wa AFIS unafanya kazi ndani ya kipindi cha miezi sita. Ripoti ilieleza mfumo wa AFIS ulikuwa unafanya kazi katika vituo 14 pekee kati ya vituo 108 hivyo agizo la kamati halikuwa limetekelezwa kikamilifu.

Spika ametoa agizo kwa serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi ndani ya miezi mitatu ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi kuwa na utambuzi wa haraka wa wahusika wa matukio ya kihalifu katika vituo vyote nchini. Pili masuala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.

Spika anatarajia sasa suala hilo litafikia mwisho na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.

TAARIFA PAC : LUGUMI HANA HATIA

TAARIFA YA SPIKA KWA UFUPI
"23 April 2016, PAC iliomba Kuunda kamati ndogo kwa mujibu wa Kanuni ya 117 fasili 18 ili kufuatilia utekelezaji wa Agizo la PAC la bunge la 10 lililotolewa tarehe 23.10.2014 kwa Jeshi la Polisi Kuhusu utekelezaji wa Mradi wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole AFPIS

Msingi wa Agizo ni Ripoti ya CAG 2012/2013 kutokana na kutokukamilika na kutokufanya kazi ipasavyo kwa mradi huo.

Kazi ya Mradi huo ilikuwa ni kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya LUGUMI ENTERPRISES LIMITED.

Polisi waliagizwa Mitambo ifanye kazi ndani ya miezi sita.

CAG aliripoti tena utekelezaji kuwa AFPIS inafanya kazi katika vituo 14 tu kati ya vituo 108

Kamati ilimtaka katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani alete taarifa ya utekelezaji. Katibu mkuu taarifa yake ikaonyesha mitambo imefungwa vituo 153 pamoja na makao makuu ya polisi tofauti na taarifa ya CAG ilivyosema.

Kamati ikaomba kuhakiki kujiridhisha na kujionea, na kamati ndogo ikaundwa kuhakiki.

HADIDU REJEAkamati ifanye uhakiki iwapo vilinunuliwa na kufungwa

kamati imemaliza kazi yake, Imeiwasilisha PAC na PAC imeijadili na kuikabidhi kwa Spika kama Kanuni zinavyotaka.

MATOKEO YA TAARIFA YA KAMATI
i. Kamati imejiridhisha kwamba VIFAA VIPO Vituo vyote 153 na makao makuu ukiacha kasoro zilizojitokeza.

ii. Kilichobaki ni vifaa hivyo kufanya kazi

Nimekabidhi matokeo (maoni, Ushauri na mapendekezo) yote ya kamati kwa serikali

AGIZO
i. Serikali ihakikishe mfumo huu unafanya kazi ndani ya Miezi mitatu kutoka leo hii ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi.

ii. Maswala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.

iii. PAC ihakikimaelekezo niliyoyatoa na baada ya uhakikikamati itoe taarifa bungeni wakati wa uwasilishaji wa taarifa yake ya mwaka.

iv. Ninatarajia sasa swala hili litafika mwisho na CAG atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha utekelezaji wa maagizo niliyoyatoa."
 
Ni baada ya Kamati ya Bunge iliyopewa kazi ya kufuatilia Sakata la Lugumi kuthigitisha kuwa vifaa mashine hizo zimefungwa katika vituo vyote. Agizo hilo limetolewa na Bunge kupitia kwa Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson wakati akiahirisha Bunge la 11 leo mjini Dodoma
Ni pure siasa za usanii....

Sasa ndiyo naanza kuelewa alikuwa na maana gani huyo Lugumi alipotamba siyo kila jipu Magu ana uwezo wa kulitumbua.......

Hivi kwa mwendo huu wa Bunge la mfumo wa Chama kimoja la huyo mdada, ni nani atathibitisha kama mashine hizo zimefungwa?

Na Je ni sheria gani ya nchi hii inayoruhusu mwizi arejeshe mali akizoiba halafu ataachiwa huru?!
 
Huyo Naibu Spika Anatafuta Marungu na Mabomu ya Mchozi tu.
 
Habari wakuu,

Leo akihitimisha bunge, naibu spika ametolea ufafanuzi utekelezaji wa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole(AFIS), hoja iliyojengwa kutokana na mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) kwa kutokamilika kwa mradi huo.

Agizo la bunge lilimtaka afisa masuhuli wa jeshi la polisi kuhakikisha mfumo wa AFIS unafanya kazi ndani ya kipindi cha miezi sita. Ripoti ilieleza mfumo wa AFIS ulikuwa unafanya kazi katika vituo 14 pekee kati ya vituo 108 hivyo agizo la kamati halikuwa limetekelezwa kikamilifu.

Spika ametoa agizo kwa serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi ndani ya miezi mitatu ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi kuwa na utambuzi wa haraka wa wahusika wa matukio ya kihalifu katika vituo vyote nchini. Pili masuala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.

Spika anatarajia sasa suala hilo litafikia mwisho na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.
 
Hakika Ccm Imechoka Tuitoe
Yaani Jambo La Kutoa Adhabu Wanampa Muda
Mahakama Ya Mafisadi Ni Kwa Wanyonge Tu
 
Back
Top Bottom