Jeshi la Polisi lasema linafanya uchunguzi kifo cha Mfanyabiashara Banjoo wa Arusha

Jeshi la Polisi lasema linafanya uchunguzi kifo cha Mfanyabiashara Banjoo wa Arusha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Jeshi la Polisi mkoani Arusha, limesema linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja aitwaye Abdilah Musa maarufu kwa jina la Banjo ambaye alifariki dunia huko katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.

Akitoa taarifa hiyo leo, Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo, amesema kuwa Jeshi hilo lilipokea taarifa kuhusiana na kupotea kwa mtu huyo Februari 13, 2026 ambaye inaelezwa alipotoea kuanzia Februari 12, 2026.

Kamanda Masejo amebainisha kuwa wakati wakiendelea na uchunguzi, februari 19, 2026 walipokea taarifa ya mtu huyo kuwa amefariki dunia huko mkoani Dodoma.

Aidha, amebainisha kuwa pamoja na taarifa ambazo wameshazikusanya na wanazoendelea kuzikusanya, ametoa wito kwa mtu yoyote mwenye taarifa ambazo zinaweza kusaidia kufanikisha uchunguzi huu, asisite kuzitoa kwani watazipokea na kuzifanyia kazi kwa haraka.

Pia soma ~ LHRC yalaani tukio la Mfanyabiashara Banjoo wa Arusha kutekwa na kuuawa
 
According to Mange Wanahusika wao. Watachunguza nini?

Wamkamushe Mange kwanza , otherwise wana pa kuanzia
 
Kwa hali ilivyochafuka kisiasa na kiusalama lazima tu watu kama hao wataanza kuwa neutralized...

Kunauoga flani sasa upo kwenye vyombo vya usalama...
 
Kifo cha Banjoo
This job can be done in less than 24 hrs. Easy , easy , easy , easy. Lakini haipaswi kufanywa na nyie Polisi kwa sababu you are suspects....,
 

Attachments

  • 20260220_213722.jpg
    20260220_213722.jpg
    158.3 KB · Views: 37
Ushaambiwa mtu jambazi..Sasa negotiation ya nini??
Tanzania ndio nchi yenye anti terrorist wenye huruma na busara...fikiri jambazi Huwa wanaonywa more than once kabla ya kutembelewa!!!

Watu wa ugaidi vivyo hivyo...Sasa ukiona adi kanyakuliwa ujue alikaidi maonyo
 
Ushapewa onyo bado unakaza shingo file lake la 2013 anastahili
 
Polisi wafanye kazi zingine za muhimu. Kifo cha muuaji ni kupoteza muda kuchunguza.
 
Back
Top Bottom