Pre GE2025 Jeshi la Polisi lazingira Ofisi ya Makao Makuu CHADEMA Mikocheni na kuzuia Mkutano wa Mnyika na Waandishi wa Habari

Pre GE2025 Jeshi la Polisi lazingira Ofisi ya Makao Makuu CHADEMA Mikocheni na kuzuia Mkutano wa Mnyika na Waandishi wa Habari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
🎺🥁 Chadema Chadema 🥁🎺 People's power🥁🎺
 
Ukisema jeshi la polisi unakosea,ccm ndio waliozuia mkutano huo kupitia matumizi mabaya ya jeshi la polisi
 
sasa hamjui hata mnyika anataka ku adress jambo gani mshazuia je kama anataka kuipongeza serikali kwa mkutano huu kabambe nchini?

SINA hakika kama na sisi tukienda kwao mambo yote yatasimama
 
Ni kama vile huo mkutano inabidi shughuli nyingine zote zisimame sijui na kwingine kunakwua hivi. Mfano kama kuna mkutano wa baraza kuu la UN pale newyork kiila jambo huwa linasimama?
Lisimame wapi? Hakuna mtu mwenye time now kwamba wanamkutano, ni Tanzania pekee tu ndipo shule zinafungwa na polisi kuzingira chama cha siasa
 
Niliwaambia kiusalama hiyo Press haitawezekana
Usalama gani unaouzungumzia,ama ni uharibifu gan ama fujo gani zingeweza kuletwa katika mkutano huo,yan ni sawa na kupewa jina la utani na ulikatae kwa nguvu ndivyo ambavyo linazidi kushika
Ukihisi C ni mwehu bas usijibizane wala kusumbuka nae maana wote mtakua wehu,
They need to chill and calm their fear/stress
 
Usiwalaumu Polisi, wao wanatekeleza maagizo tu na hata wao hawana uwezo wa kukataa. Lawama ziende kwa waliowaagiza
Polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria. Wanafuata sheria au wanafuata maagizo?

Ndio maana wakipelekwa kwenye uga wa sheria wana chimba
 
Kwa jinsi tech ilivyo, hakuna haja ya kukutana na hao waandishi. Zoom meeting nk si zipo, wafanye online meeting warushe online watu wapate habari, after all, ni press.
Hata hao marais wangeweza kufanya zoom meeting.
 
YAANI CHADEMA KUACHA UJI NI KAZI SANA LABDA HUO UJIN UANZE KUWAOMBA HELA, HIVI KWELI UNAONA KABISA KUNA UGENI WA KITAIFA MNAFANYA PRESS YA NINI MNASHINDWA KUVUMILIA SIKU MBILI NDIYO MUANZE HUO UJI WENU? HAMNA ADABU KABISA
Ukaandika kwa herufi kubwa kabisa.Na vyuo je?
 
Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezuia mkutano wa waandishi wa habari wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Mnyika uliopangwa kufanyika leo Jumatatu 27/1/2025 saa tano asubuhi.

View attachment 3215420

Nje ya jengo la Makao Makuu hayo wapo askari wa jeshi la polisi kwa taarifa tulizonazo waandishi wa Jambo TV, Azam TV, Mwananchi wamezuiwa na kuondolewa eneo hilo.

View attachment 3215428

Aidha sababu zinazoelezwa juu ya kuzuiwa kwa mkutano huo inadaiwa ni uwepo wa Mkutano wa Kimataifa wa Nishati (M300). Huku ikielezwa kuwa mkutano huo wa CHADEMA ungeweza kusogezwa mbele na kufanyika kuanzia tarehe 29.

View attachment 3215422

Pia, Soma: Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika kuongea na Waadishi wa Habari Makao Makuu ya Chama, Mikocheni
Tuna upumbavu wa hali ya juu sana
 
Kweli samia hana hoja, yaani anataka kila kitu kisifanyike ili atangazwe yeye tu. Fungeni maduka na baa zote nchi nzima
 
Back
Top Bottom