Jeshi la Polisi limeichafua taswira ya Tanzania kwa kuzuia kongamano la CHADEMA na kuwakamata viongozi wake wakuu

Jeshi la Polisi limeichafua taswira ya Tanzania kwa kuzuia kongamano la CHADEMA na kuwakamata viongozi wake wakuu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Jana taswira ya Tanzania imechafuliwa na Jeshi la polisi kwa kuzuia kongamano la CHADEMA na kuwakamata viongozi wake wakuu wote.

Kongamano kama hilo la vijana wa CHADEMA limeshafanywa na vyama vingine kama CCM na ACT Wazalendo bila shida.

Jana vyombo vyote vikubwa vya kimataifa vimeripoti kitendo cha aibu kulichofanywa na polisi Mbeya. NGOs za ndani na za nje zimelaani kitendo kile. Taasisi za kidemokrasia na haki za binadamu za ndani na nje zimelaani tukio lile. Kwa ufupi nchi imeonekana haina utulivu wa kidemokrasia na kisiasa kwa tukio lile.

Kama kutakuwa hakuna uwajibishwaji wa viongozi wa jeshi la polisi kwa kadhia ile basi moja kwa moja itaonekana lilikuwa ni agizo la rais lakini kama sivyo lazima hatua zichukuliwe kwa aibu ile. Kama mama anahusika au hahusiki lakini tayari zile 4R zake zimeshachafuliwa.

Kuna haja pia ya kumuwajibisha msajili wa vyama vya siasa kwani naye amekuwa kikwakwazo kwa vyama vya siasa kufanya shughuli zake kwakuwa na yeye kajigeuza polisi au waziri kwa kuzuia na kuingilia shughuli za vyama vya siasa.

Hapa niwapongeze kwa dhati Wasafi FM kwenye kipindi chao cha leo asubuhi cha uchambuzi wa magazeti kwa namna walivyolidadavua suala hili kwa uwazi, ukweli, bila woga wala upendeleo. Hongera sana Zembwela, Gerald Hando na Maulidi Kitenge. Mmekitendea haki kile kipindi. Kweli ninyi ni wazaee wa minyama.

Vile vile nampongeza katibu mkuu wa CCM kwa busara kubwa alizozionesha kwa kushauri viongozi wa CHADEMA waachiwe. Mara zote Dr. Nchimbi amekuwa, mtulivu, hana mihemko, busara, mkweli na muwazi katika kukemea hata kauli za hovyo za viongozi wa CCM kama zile zilizotolewa na kiongozi wa UVCCM kagera na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara.

Katika misingi ya utawala bora na uwajibikaji ilipaswa hapa waziri wa mambo ya ndani, IGP na RPC Mbeya wajiuzulu. Hilo kwa nchi hii labda mpaka atakaporudi Yesu

Shame on you polisi Mbeya na wote walioshiriki kuvuruga utulivu wa nchi jana.
 
Kitendo hiki cha aibu na fedheha kilichofanywa na Jeshi la Polisi hakikutokea kwa bahati mbaya hata kidogo bali ni lile fukuto ambalo liko ndani ya CCM la kundi ambalo tangu awali halikumkubali Samia kuwa Rais na hatimaye halikupenda kabisa maridhiano ya CCM na Chadema. Wahafidhina hawa wamekuwa na donge na aina ya uongozi wa Rais Samia na hasa alivyokuwa anamiminiwa sifa kutoka ndani na nje ya nchi jinsi alivyoweza kuongoza nchi bila mifarakano kati ya CCM na wapinzani.

Wahafidhina hawa na haters wa Samia wameamua kulitumia jeshila polisi kuharibu taswira ya Rais na uongozi wake kwa kujifanya wanataka kutengeneza mazingira mazuri ya ushindi wa CCM kwa kuinyamazisha kabisa Chadema kueleka chaguzi zijazo ili CCM ipate ushindi wa kishindo lakini nyuma ya pazia wakijua madhara ya kutumia Polisi ni kumchafua Rais.
 
Back
Top Bottom