Polisi Tanzania yatoa taarifa juu ya matukio matatu ya watu kutekwa na kuuawa
Chanzo cha picha,Jeshi la Polisi Tanzania/X
Polisi nchini Tanzania imetoa taarifa kuhusu watu matukio ya watatu walioteka na kuuawa, katika mazingira ya kutatanisha nchini humo.
Hii imekuja baada ya hivi karibuni baaadhi ya jamaa wa watu waliopotea nchini Tanzania kuisimulia
BBC kuhusu jinsi ndugu zao walivyopoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo hii leo, inamhusu kijana Samwaja Sifaeli Said, mwanye umri wa miaka 22, aliyetoweka tarehe 8 Agosti, 2024 Singida Tanzania, na mwili wake kupatikana ukiwa umefunikiwa kwenye shimo, huku sehemu zake za siri zikiwa zimekatwa.
Kufuatia mauji ya Samwaja Sifaeli Said, taarifa hiyo inasema, wameweza kuwakamata vijana wawili ambao walikwenda kunywa pombe na marehemu, na baada ya mahojiano ‘‘waliielezea polisi kwamba ni kweli walikwenda kunywa pombe na marehemu na walipokuwa wanarejea walimuua kwa kumyonga na kisha kumkata sehemu zake za siri’’
Polisi imeendelea kusema kuwa watuhumiwa waliieleza kuwa walielezwa na mganga wa kienyeji kuwa wakipata sehemu za siri za binadamu watakuwa matajiri.
Baadaye watuhumiwa waliwaonyesha polisi mwili ambao ulitambuliwa kuwa ni wa Samwaja Said Raphael.
Polisi imetaja tukio la pili linalomhusu muathiriwa mwanamke kwa jina la Ezenia Stanley Kamana mwenye umri wa miaka 32, Mkazi wa Tandika Magorofani jijini Dar es Salaam, ambaye alitekwa/ kutoweka.
Imesema baada ya uchunguzi wake ilibaini kuwa marehemu alikuwa na rafiki yake wa kiume kwa jina Abdalla miraji@ mussa ambaye alikana kuwa na marehemu, lakini baada ya polisi kufanya uchunguzi na kupatikana kwa viungo vya marehemu, mshukiwa alikubali kuwa alimuua mpenzi wake.
Aidha tukio jingine lililotajwa na polisi katika taarifa hiyo ni la mtoto Elia Elfaza
Raymond Mchome mkazi wa wilaya ya Handeni Tanga mwenye umri wa miaka 3 , aliyetoweka tarehe 9 Agosti, 2024 wakati alipokuwa anacheza nje.
Polisi inasema baada ya uchunguzi wa tukio hilo ilifanikiwa kumkamata mshukiwa Jackson Elisante @ Maeda mkazi Kwadjava Tanga mwenye umri wa miaka 23. Baada ya kuhojiwa mshukiwa akiliri kuwa mtoto huyo kumfukia ndani ya chumba anachoishi, polisi imesema katika taarifa yake.
Watuhumiwa wengine wawili bado wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
Polisi imetoa rai kwa viongozi wa kidini, wazee wa kimila , wananchi na wadau mbali mbali kushirikiana kuzuia ‘‘ matatizo haya yanayotokea ndani ya jamii’’
Polisi imewatahadharisha baadhi ya wananchi wenye tabia ya kujichukuliwa sheria mkononi, kufahamu kuwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria. chanzo.BBC