Jeshi la Polisi limewakamata na kuwahoji waliovunja vioo Treni ya SGR, ni watoto wa miaka 12 na 16

Jeshi la Polisi limewakamata na kuwahoji waliovunja vioo Treni ya SGR, ni watoto wa miaka 12 na 16

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Hii taarifa mbona kama ya kutuzuga hivi? Hayo mawe yalikuwa ya ukubwa kiasi gani mpaka yavunje hivyo vioo? Au ni sababu ya mwendo? Wazee wa physics mje mtueleze.

Lakini pia kama walikuwa wanashindanisha kasi siyo kwamba yangerushwa kwenye uelekeo ule treni inakoenda kuona kipi kitawahi kufika, au ndio yalikata kona kama ile risasi iliopigwa juu karibu na kituo ikarudi chini hadi kumpata mwanafunzi aliyekuwa anajaribu joho, au risasi iliyppigwa juu ikakata kona hadi kumfikia Akwilina?

Mapovu yenu chawa myaache kwenye nguo, mwenye ana majibu ya kitaalamu kuelezea hilo atuambie tuelewe.

=====

Baada ya kufanya msako Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watoto hao wawili ambao wote wakazi wa kijiji cha Manase Wilaya Chamwino.

Chanzo cha kufanya uharibifu huo ni baada ya kuona treni ikipita wakarusha mawe kwa pamoja ili kuona kama mawe waliyoyarusha yataweza kushindana na mwendo wa treni.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na njia hiyo ya treni kupeana elimu juu ya ulinzi wa miondombinu hiyo na kwa wazazi kutoa elimu kwenye familia hasa kwa watoto kuacha vitendo vitakavyosababisha uharibifu na hivyo kukinzana na sheria za nchi.

Screenshot_20241124_091350_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom