Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema kuanzia sasa Madereva wanaoendesha magari kwa mwendokasi na kusababisha ajali watawekwa mahabusu na kupelekwa Mahakamani moja kwa moja na siyo kulipa faini tena.
Kamanda wa Polisi Wilbroad Mutafungwa amesema hayo wakati wa mazungumzo yake na Madereva katika kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli na kusisitiza kuwa “dereva atakayekutwa anaendesha gari kwa mwendo kasi na kuyapita magari mengine bila kufuata sheria za barabarani atachukuliwa leseni yake na kupelekwa mahabusu kisha Mahakamani na sio kulipa faini kama ilivyozoeleka”.