BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amewataka madereva Bodaboda wa Jijini Mbeya kushiriki mafunzo ya udereva katika vyuo vilivyosajili na kutambulika kisheria na kuhitimu ili waweze kupata leseni ya udereva.
Ameyasema hayo Aprili 03, 2023 katika kikao kazi cha uongozi wa Bodaboda wa Jijini Mbeya kilichofanyika katika uwanja wa FFU Mbeya.
Kamanda Kuzaga amesisitiza kuanza Aprili 04, 2023 kila dereva Bodaboda kuwa na kofia ngumu (Helmet) mbili kama sheria na masharti ya mtumiaji wa chombo hicho wanavyoelekeza.
Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya SP Yusufu Kamotta amesisitiza suala la kila Bodaboda kujisajili katika kijiwe chake ili kutambuana na kuwabaini wahalifu.
Aidha amewataka madereva Bodaboda wa Jijini Mbeya kuheshimu sheria zote za Usalama barabarani ikiwemo kuwa na leseni ya udereva, kukata bima ya chombo cha moto, kuvaa kofia ngumu.
Dawati la Habari Polisi Mbeya