Jeshi la Polisi mjitathimini na kuwajibika kwa kuzingatia haki na usawa katika jamii. Mnafanya kazi na watu na nyie ni watu

Jeshi la Polisi mjitathimini na kuwajibika kwa kuzingatia haki na usawa katika jamii. Mnafanya kazi na watu na nyie ni watu

MKAKA HALISI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2018
Posts
631
Reaction score
1,263
Ni ukweli usiopingika kuwa huku mtaani tunao Hamza wengi sana ambao wengi wao ni matokeo ya utendaji kazi wenu unaobeba maslahi ya wachache na kuacha kundi kubwa likisononeka na Dunia ya sasa taarifa zinasafiri kwa haraka sana hivyo mengi tunayaona na inasikitisha zaidi pale viongozi mnakuja na majibu mepesi kama nyie ni watu tofauti na jamii mnayoihudumia na mnasahau kuwa nyie polisi mnatokana na sisi Raia.

Lakini sio polisi tu wapo pia TRA inasikitisha kuwa umewekwa kwaajili ya kutoa huduma kwa mwananchi lakini huyo mwananchi unamhudumia kama hakustahili kupata huduma stahiki hivyo anapaswa kushukuru kwa kila jambo na hapaswi kuhoji wala kuuliza chochote bali akuache wewe ufanye yako mpaka ulivyopanga wewe mkumbuke kuwa Tanzania ni yetu sote haki na usawa huinua Taifa.
 
Mfano huo hapo

 
Wakikusikia bila damu masikioni usiache kutuletea mrejesho
 
Back
Top Bottom