Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limewakamata Watuhumiwa watatu kufuatia mauaji ya aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limewakamata Watuhumiwa watatu kufuatia mauaji ya aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Naona Polisi lipo na kasi ya 5G kuwakamata watuhumiwa waliofanya makosa kwa viongozi wa CCM ila upande wa vyama vingine uchunguzi unachukua muda mrefu sana.

Kwani kuna siri gani kwenye chunguzi zao?
================

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa Limesema limewakamata Watuhumiwa watatu kufuatia mauaji ya aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa aliyeuawa kwa kupigwa Risasi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Allan Bukumbi amesema tayari Watuhumiwa watatu wamesha kamatwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa Mahakamani kwaajili ya hatua zaidi za kisheria.

“ Kiukweli tukio la Katibu wa CCM linaendelea Vizuri na tumeshawakamata Watuhumiwa kadhaa na wengine baada ya kubaini kuwa hawahusiki basi tuliwaachia ila upelelezi Bado unaendelea na hatua za mwisho zikikamilika basi tutawataarifu “ Amesema Allan Bukumbi

Soma Pia:
Ikumbukwe tarehe 13 November Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilolo Christina Kibiki aliuawa kwa kupigwa Risasi na Watu ambao hawakufahamika nyumbani kwake.

 
Back
Top Bottom