Na Thompson Mpanji,Mbeya.
JESHI la Polisi mkoani Mbeya limeanza kupambana na wanaokaidi maelekezo ya wataalamu wa Afya katika mapambano dhidi ya COVID-19.
Mwandishi wa Habari hizi ameshuhudia Baadhi ya Askari wa Jeshi hilo Kikosi cha Usalama Barabarani katika vituo vya Nane Nane na Iwambi jijini Mbeya wakisimamisha basi za abiria maarufu dala dala na kushuhudia wakiwashusha baadhi ya abiria ambao hawajavaa kifaa kikinga mdomo na pia(Barakoa).
Aidha katika kuzingatia maelekezo ya social distance, Askari hao wameonekana wakiwashusha abiria waliozidi idadi na kubanana katika mabasi hayo huku madereva wa mabasi hayo wakionywa.
Hivyo wananchi wa Mkoa wa Mbeya wanapaswa kizingatia maelekezo na miongozo inayotolewa na Viongozi wakuu wa Nchi na Viongozi wa dini pamoja na wataalamu wa Afya.