Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Takwimu za Hali ya Uhalifu nchini Tanzania zimeonesha kati ya Januari 2023 hadi Desemba 2023 kulikuwa na Matukio 3,778,908 ya Jinai na Usalama Barabarani yaliyoripotiwa katika Vituo vya Polisi ikiwa ni ongezeko la Matukio 658,825 (21.1%) kutoka matukio 3,120,083 ya mwaka 2022.
Ripoti ya Jeshi la Polisi imeonesha Makosa ya Ubakaji yaliongezeka kutoka 6,828 mwaka 2022 hadi 8,691 mwaka 2023, Ulawiti uliongezeka kutoka makosa 1,586 hadi 2,488, Wizi wa Watoto na Kutupa Watoto uliongezeka kutoka matukio 228 hadi 259.
Aidha, Makosa Madogo 553,462 ya Jinai yaliripotiwa zaidi katika Maeneo 5 ya Nchi ambayo ni Kinondoni (57,404), Mwanza (47,220), Ilala (36,806), Temeke (34,500) na Morogoro (30,474).
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania