GE2025 Jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi Morogoro limefanya mazoezi ya pamoja kuimarisha ushirikiano na usalama kwa jamii

GE2025 Jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi Morogoro limefanya mazoezi ya pamoja kuimarisha ushirikiano na usalama kwa jamii

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
MAZOEZI YA PAMOJA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA USALAMA KWA JAMII

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama limefanya mazoezi ya pamoja ya kutembea na kukimbia kuzunguka maeneo mbalimbali ya mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa himaya na kuimarisha ushirikiano.

Soma pia: Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Katavi vyashiriki mazoezi ya pamoja


Akizungumza na Usalama TV baada ya mazoezi hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro alieleza kuwa lengo kuu la mazoezi hayo si kuwatisha wananchi, bali kuimarisha usalama, kuonesha mshikamano wa vyombo vya ulinzi, pamoja na kuwa karibu na jamii.

Kamanda alibainisha kuwa mazoezi hayo hutoa nafasi ya kufahamu mazingira, kuhamasisha utimamu wa miili ya askari, na kuhakikisha vyombo vya ulinzi vinaendelea kushirikiana kwa ukaribu katika kulinda amani na mali za wananchi.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa za kiuhalifu na kusaidia kudumisha utulivu katika maeneo yao.
 
Hii nchi ukipata upenyo wa kuhama fanya chapu

Nchi ya kingese sana hii kwa mtu mwenye akilii kubwa hutoboi!
 
Back
Top Bottom