PostGE2025 Jeshi la polisi Tabora: Matishio yamejitokeza ila mkoa umebaki salama, kwasababu Wananchi hawataki vurugu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limewahakikishia wananchi kwamba usalama wao utakuwa wa kimsingi katika sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Richard Abwao, amesema jeshi hilo litaendesha doria katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wananchi washerehekee sikukuu hizo kwa amani na utulivu.

Kuhusu matishio amesema "Matishio yamejitokeza lakini kwa mkoa wa Tabora tumeendelea kuwa salama, tumekuwa salama kwasababu wananchi hawataki vurugu, na wananchi wako tayari kushirikiana na Vyombo vyao vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kwamba tunakuwa na Amani, na Usalama wakutosha"

Wakati anaongea hivyo huyo askari feki unakuta tumbo limejaa rushwa, uharo mtupu.

Huyo askari feki ni mhalifu kama walivyo majizi mengine yanayojiita wanasiasa.
 
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limewahakikishia wananchi kwamba usalama wao utakuwa wa kimsingi katika sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Richard Abwao, amesema jeshi hilo litaendesha doria katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wananchi washerehekee sikukuu hizo kwa amani na utulivu.

Kuhusu matishio amesema "Matishio yamejitokeza lakini kwa mkoa wa Tabora tumeendelea kuwa salama, tumekuwa salama kwasababu wananchi hawataki vurugu, na wananchi wako tayari kushirikiana na Vyombo vyao vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kwamba tunakuwa na Amani, na Usalama wakutosha"

Maajabu Tabora hadi kuna maghorofa na lami?
 
Back
Top Bottom