Pre GE2025 Jeshi la Polisi: Tumepata taarifa CHADEMA wanapanga Maandamano na Kuvamia Vituo vya Polisi Dar kwa wakati mmoja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hawa Polisi wanachekesha, wameshindwa kubaini kwamba mganga tu wa jadi ameua na kuzika watu 6 katika mikoa 2 tofauti ,mkoa mmojawapo ni makao makuu ya nchi, leo intelijensia yao inatueleza chadema wanataka kuvamia vituo vya Polisi !? Kwanini itelijensia ya Polisi inatumika ikitokea kuna jambo la chadema kwwingineko haitumiki!? Chadema waliwahi kufanya nini jambo Zito la kutishia usalama wa nchi!? Wanaogopa kivuli chao na wamejipanga kisiasa zaidi
 
Wameona hizi story za kuchomekea kuhusu vifo vya watu kwa waganga bado haziondoi ukweli wa madai ya cdm kuhusu kutekwa wanachama wake. Sasa wanatengeneza propaganda mfu ili wahadae umma na hatimaye watu waone cdm ni chama hatari.

Ukweli ni kuwa madai ya cdm kuhusu makada wake kutekwa ni ya kweli, na wahusika ni hao vyombo vya dola hasa tiss, kupitia sheria mpya ya usalama wa Taifa.
 
Polisi inadhalilisha Taifa, mbinu zake ni duni mno! yaani hata kutengeneza uongo hawawezi yaani!
 
Nilidhani Polisi wanatoa tamko kuhusu wajibu wao wa kuwatafuta waliotekwa nyara....

Inahitaji akili ya F nne kuelewa maana ya taarifa hii ya polisi.

Mungu ibariki Tanzania
 
Wapendwa
Ni wakati wa selfe defence.

Msikamatwe kama kuku
 
TANPOL wanwabagua CDM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…