Jeshi la Polisi: Tunafuatilia kutoonekana kwa bwana Danstan Daud Mutajura

Jeshi la Polisi: Tunafuatilia kutoonekana kwa bwana Danstan Daud Mutajura

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Januari 04,2025 majira ya saa 8:00 mchana lilipokea taarifa toka kwa wananchi ya kuonekana kwa gari aina ya Mercedes Benz lenye namba za usajili T 109DVY likiwa limetelekezwa eneo la BUZA SIGARA. Taratibu zilifanyika na gari hilo kuvutwa hadi kituo cha Polisi BUZA.

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Aidha tarehe 05 Januari 2025 katika Kituo cha Polisi Changombe zimepokelewa taarifa kutoka kwa ndugu kuwa gari hiyo iliyotelekezwa ilikuwa inaendeshwa na ndugu yao aitwaye DASTAN DAUD MUTAJURA ambaye toka Januari 4,2025 alipoondoka kuelekea katika shughuli zake hajarejea nyumbani. Ufuatiliaji zaidi wa kutoonekana kwa bwana Dastan Daud Mutajura unaendelea.

View attachment 3192979

Soma Dunstan Daudi Mtajura adaiwa kutekwa eneo la Buza
What a crap! Mnamtafutaje? Kule Somali, kuna methali inasema, "ngamia aliyeibiwa na Mwenyewe, hawezi, kupatikana?
Kijana alikuwa TISS,kapotea, eti anatafutwa na polisi hawa makanjanja?!
 
Back
Top Bottom