LGE2024 Jeshi la Polisi wamkamata Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Songwe sababu hazijafahamika

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Jeshi la Polisi wamemkamata Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Songwe Ezekia Zambi kwa sababu ambazo bado hazijafahamika.

ACT Wazalendo Vwawa iliruhusu Chadema kutumia ratiba yake kufanya mkutano wa Mwenyekiti Freeman Mbowe lakini polisi wakazuia.

Soma Pia: Freeman Mbowe akamatwa na Jeshi la Polisi akielekea Mbozi mkoani Songwe

1732285800309.png

Source: Jambo TV
 
Habari za usiku huu waungwana. Bila kuchelewa niende moja kwa moja kwenye maada.

Hii sio sawa kwakweli, heshima ni kitu cha bure. Inakuwaje mtu mkubwa kama Mbowe kukamatwa na askari kuhamishwa kwenye gari lake na kukandamizwa kwenye kalandinga namna hii? Hawa polisi wanatumwa ndio. Lakini ni vema wakaangalia na kufanya kazi yao kwa weledi.

Sio kwa namna wanavyo fanya, maana hata kama wanatumwa wakumbuke kibao huwa kinageuka.

Nawasilisha.
 
Picha iko wapi?
 
Mtu mkubwa kama Mbowe!
Kumbe Mbowe amewazidi watanzania wote kwa umri?
 
Laana ya Zito Kabwe kushangilia kifo cha Magufuli naiwatafune.

Mlishangilia eti mtapumua kiko wapi sasa
Ni kweli kabisa huwa nawashangaa sana hawa wapinzani ni wapoombuvour sana . Yaani mtu anatumia muda mwingi kumshambulia Magufuli ambaye wananchi 80 % ya Watangayika wanakumbuka na walimwamini tangu akiwa waziri kwa kila wizara aliyopelekwa.

Sasa hawa wapinzani Muvee 💩💩 wanapoteza sana kura na kwa watu . Watu wameshaanza kuwaona kuwa CCM na wapinzani wote ni sawa na wote ni wezi wanaotaka kupata fursa za wizi.

Hivi mtu gani mwenye akili timamu atamlinganisha Huyu Dr .wa kichina na Dr. Magufuli kwenye kulinda na kutetea rasilimali za Tanganyika .
Hivi kwa mtu mwenye akili timamu hata kama alikua anamchukia marehemu si bora akae kimya ? Utasimamaje kwenye nchi yenye ufisadi mkubwa kama Tanzania umponde Magufuli kwa sasa kama sio kujiua kisiasa.

Nadhani hapo imebaki tu kidogo aje mzalendo mmoja aliyevaa Unifomu ya kitenge cha mabaka mabaka afute hata Siasa zote za vyama vyote mana ,kilichopo madaraka ni cha matapeli na wezi cha wapinzani ni wapambe wa matapeli na kukwamisha juhudi za wazalendo kuingia ikulu .Wapinzani walitumikia kumzuia Lowasa kuingia Ikulu . Leo hii Maji ya Ziwa viktoria yangekuwa yamefika Gairo na Loliondo ingekua umerejesha kuwa eneo la Tanganyika na Wamasai wangeishi Tanganyika badala ya kwenda kujifunza ushougour kwa watalii wa Kigiriki kule kwenye visiwa vya Qaroufou.
 
Mbona ni jambo la msingi sana kwa hawa wapinzani Maslahi koko kupata kipigo cha mbwa quoquo .
Au mlitaka nani apigwe kama sio mpuuzi mmoja na genge lake lisilo na uelekeo wala tija kwa siasa za mageuzi zaidi ya kutumia siasa kupiga pesa na kula rushwa za watawala huku wanyonge wakikosa mageuzi ya Kweli kwenye nchi .

Hivi kwa Mwana siasa mwenye kujua kuwa watanzania Tangu mwaka 1995 walikua wanataka mabadiliko na kupinga ufisadi wote chini ya NCCR mageuzi ya Mrema mpinga magobachori atapata vipi shida ya kuikabili CCM iliyokataliwa tangu miaka 32 imiyopita.

Nini kinadhoofisha mageuzi au demokrasia hasa ya kupiga kura kama sio wapinzani wenyewe ?

Mwenyekiti amekamatwa wa chama chenye wanachama zaidi ya mil. 8 halafu Kuna msemaji wa chama amejificha darini au uvunguni mwa kitanda cha anatuma kimemo analiomba jeshi la polisi eti limwachie haraka .

Blaliful !!! Hapa mnategemea mageuzi au kugeuzwa nyie.!!
Wajeenger kabisa !!!
.Yaani tulitegemea Mrema awatoe wanachama mil. 8 wote wakajiunge na mwenyekiti wao huko polisi na magerezani na wakatae kabisa kuachiwa . Yaani wagome kutoka ndani hata kwa dhamana . Wakatae dhamana na pasiwe na mtu wa kuwawekea dhamana na wakitaka kuwatoa ndani wakatae waombe kwenda gerezani na huko wakatae kupewa dhamana ili kwa mara ya kwanza mabomu yapigwe ndani ya mahabusu kuwalazimisha watu kutoka vifungoni .Je,serikali itawafungulia kesi watu mil. 8 na kuwafunga gerezani kwa kosa la kukataa kutoka kwenye mahabusu au gerezani?

Kwa sababu CCM inatumia polisi kuwatisha kwa sababu mnaogopa kulala ndani wakati kifo cha wengi ni harusi.

Nendeni mkashangilie na kuandamana ndani ya lokapu ili dunia ione kuwa kweli mnapigania demokrasia ya kweli sio blablah za kuogopa kukamatwa hadharani bila kosa . Huna kosa unaogopa nini kukaa hata gerezani .?

Walevi na wahuni wakubwa ndio maana hata mbinu zenu hazileti mwamko wa kimapinduzi mpaka sasa Watumishi wa Mungu ndio wanapigania uhuru wenu nyie wanasiasa mliojaa hila na usanii huku mkiwa lnakesha kwenye starehe wakati kuna watu wanaumizwa na kufa kwa ajili ya kujenga vyama vyenu?

ACT wameanza kutambua nguvu za kumtanguliza Mungu kwenye wakati huu wa utawala wa giza.

Nyie akina wa Chadema endeleeni kukesha na KVanti na watoto halafu mnataka kuwa juu ya nchi muwatawale wafu na rasilimali zilizoumbwa na Mungu wakati shetani aliona zikiumbwa na akatamani sana yeye ndio apewe nafasi ya kujiundia utawala wake na mifumo na majeshi yake na ukuu heshima kubwa kama alivyopewa binadamu !?
Lisu na Mbowe acheni kulewa kabla ya kupanda kwenye majukwaa mnapoteza nguvu za kiroho.
Mbowe acha starehe za kitoto huu ni wakati wa kujitenga na anasa na kujiweka wakfu kwa Mungu na hata mizimu ya Tanganyika ili kuinua roho za ujasiri na haki kwa Taifa .
Vinginevyo mtapata tabu sana na mtapigwa kipigo cha mbwa koko.
 
Hahaha ACT ndio mdudu gani Akiondoka CCM Tuachieni sisi(ACT).
 
PHEW!
Nimekosa alama sahihi ( kati ya zilizopo) ya kuweka kwenye bandiko hili baada ya kulisoma. Kwenye aya za mwanzo kabisa nilikuwa nashangaa ni nini kilicho mpata mwandishi hadi kubadilika na kuwa na fikra za namna ile; kwani mara nyingi humsoma tofauti na ilivyo kuwa kwenye aya hizo.
Lakini kadri nilivyo endelea kusoma, humo katikati ya andiko lenyewe, nikatamani niishie hapo na kulipa andiko hilo alama ya 'love' hata kabla sijamaliza kusoma andiko zima.
Nikaona nijipe moyo, nisome lote hadi mwisho kabla ya kuamua nitoe alama ipi.
Huku mwisho, pamoja na kuwa bado nina kumbukumbu ya kilicho andikwa humo katikati, nikazidi kuchanganyikiwa; ingawaje 'theme' ya maneno mazito yaliyo tumika hapo katikati ikiwa bado inatawala akili zangu!

Kwa hiyo, siwezi kutoa alama ya "Mshangao, au Masikitiko, ama ya Huzuni na wala siyo ya "Kutopenda" andiko hili

Ila bado naona uzito mkubwa wa ujumbe ulio bebwa ndani yake.

Kwa mfano: Kama kweli CHADEMA wanao wanachama wao milioni nane (milioni 8); ongeza kwenye namba hiyo na wapenzi tu wa chama hicho, ambao siyo lazima wawe wanachama.... Unaelewa maana ya kuwa na wafuasi kiasi hicho? Ummati wa watu hawa; hata kama kati yao wawe milioni tatu tu hivi, ambao kwa kila hali wapo kupigania chama chao----. Unaelewa kinachofikiriwa hapa?

Sasa basi, kama hawa watu hawastuki, wala hawajisumbui kabisa hata wakati viongozi wao wanapo pata masaibu, tena kwa uonevu kabisa; tuwachukulie vipi wanachama na wapenzi hawa wa chama?
Ni nani alaumiwe hapa, wanachama kukosa mwamko, au viongozi kutowaamsha wanachama wao waone kwamba wanayo nguvu ya kupigania haki zao na viongozi wao!

lakini dalili zimeanza sasa kubadilika kidogo, hasa kutokana na uchafu mwingibunao fanywa na viongozi wa CCM na pia baadhi ya viongozi ndani ya CHADEMA kuanza kuonyesha dalili za kuaminiwa na wanachama wao na waTanzania kwa jumla

Mwisho, nirudi kwa mwandishi wa andiko, mkuu '1000Digits'. Napenda kukupongeza kwa fikra ulizo wasilisha kwenye andiko hilo. Sisi sote, kutokana na 'frustrations' za kutojuwa nini cha kufanya mbele ya majaribu makubwa haya yanayo letwa na CCM na vyombo vyake vya dola, mara nyingi hujikuta tunalaumu, hata wakati hatuna njia za kushauri kipi kifanyike kuyaondoa haya yanayo chafua nchi yetu.

Natoa 'love' mbili mfululizo kwa andiko la mkuu 1000 digits'.
 
Sasa hawa wapinzani Muvee 💩💩 wanapoteza sana kura na kwa watu . Watu wameshaanza kuwaona kuwa CCM na wapinzani wote ni sawa na wote ni wezi wanaotaka kupata fursa za wizi.
Iwe ni kweli au siyo kweli, tatizo lipo hapa. CHADEMA na wengineo wanaweza wasikubali; lakini 'perception' waliyo nayo waTanzania wengi ni hiyo. Taratibu inaanza kuondoka; hasa kutokana na wanayo yaona yakitokea huko CCM kwenyewe.
Chama kinapo kuwa na viongozi kama Mchungaji Msigwa, na wengi wengine wa aina hiyo ambao bado wamo humo, ni kazi ngumu kuwafanya wananchi waone kuwa chama hicho kina maslahi ya nchi.
Mfano wa Magufuli ni sahihi kabisa kama ulivyo uweka; pamoja na kwama ni mfano wenye utata mkubwa kutokana na tabia zake mbovu.
Lakini wananchi waliziweka pembeni tabia hizo kwa matumaini ya yale mengine yaliyo onekana ni kwa manufaa ya nchi.
 
Hivi kwa mtu mwenye akili timamu hata kama alikua anamchukia marehemu si bora akae kimya ? Utasimamaje kwenye nchi yenye ufisadi mkubwa kama Tanzania umponde Magufuli kwa sasa kama sio kujiua kisiasa.
Hata sijui nitaku'quote' mara ngapi leo.
Lakini hapa nimeshindwa kujizuia; kwa sababu mifano halisi ipo, ya watu hao unao uliza kama wapo.
Ngoja nikutajie baadhi yao tu: Profesa wa Jalalani, a.k.s Kabuki kalamaganda; akina Bashite, si hao hapo? Akina Mkumbo, na wengi wengineo.
Ndiyo maana sasa wananchi wametambua kwamba hakuna tofauti kati ya CCM ya Samia na wengi wa hawa waliopo kwenye vyama vya upinzani

Sitaku'quote' tena.
 
Back
Top Bottom