PHEW!
Nimekosa alama sahihi ( kati ya zilizopo) ya kuweka kwenye bandiko hili baada ya kulisoma. Kwenye aya za mwanzo kabisa nilikuwa nashangaa ni nini kilicho mpata mwandishi hadi kubadilika na kuwa na fikra za namna ile; kwani mara nyingi humsoma tofauti na ilivyo kuwa kwenye aya hizo.
Lakini kadri nilivyo endelea kusoma, humo katikati ya andiko lenyewe, nikatamani niishie hapo na kulipa andiko hilo alama ya 'love' hata kabla sijamaliza kusoma andiko zima.
Nikaona nijipe moyo, nisome lote hadi mwisho kabla ya kuamua nitoe alama ipi.
Huku mwisho, pamoja na kuwa bado nina kumbukumbu ya kilicho andikwa humo katikati, nikazidi kuchanganyikiwa; ingawaje 'theme' ya maneno mazito yaliyo tumika hapo katikati ikiwa bado inatawala akili zangu!
Kwa hiyo, siwezi kutoa alama ya "Mshangao, au Masikitiko, ama ya Huzuni na wala siyo ya "Kutopenda" andiko hili
Ila bado naona uzito mkubwa wa ujumbe ulio bebwa ndani yake.
Kwa mfano: Kama kweli CHADEMA wanao wanachama wao milioni nane (milioni 8); ongeza kwenye namba hiyo na wapenzi tu wa chama hicho, ambao siyo lazima wawe wanachama.... Unaelewa maana ya kuwa na wafuasi kiasi hicho? Ummati wa watu hawa; hata kama kati yao wawe milioni tatu tu hivi, ambao kwa kila hali wapo kupigania chama chao----. Unaelewa kinachofikiriwa hapa?
Sasa basi, kama hawa watu hawastuki, wala hawajisumbui kabisa hata wakati viongozi wao wanapo pata masaibu, tena kwa uonevu kabisa; tuwachukulie vipi wanachama na wapenzi hawa wa chama?
Ni nani alaumiwe hapa, wanachama kukosa mwamko, au viongozi kutowaamsha wanachama wao waone kwamba wanayo nguvu ya kupigania haki zao na viongozi wao!
lakini dalili zimeanza sasa kubadilika kidogo, hasa kutokana na uchafu mwingibunao fanywa na viongozi wa CCM na pia baadhi ya viongozi ndani ya CHADEMA kuanza kuonyesha dalili za kuaminiwa na wanachama wao na waTanzania kwa jumla
Mwisho, nirudi kwa mwandishi wa andiko, mkuu '1000Digits'. Napenda kukupongeza kwa fikra ulizo wasilisha kwenye andiko hilo. Sisi sote, kutokana na 'frustrations' za kutojuwa nini cha kufanya mbele ya majaribu makubwa haya yanayo letwa na CCM na vyombo vyake vya dola, mara nyingi hujikuta tunalaumu, hata wakati hatuna njia za kushauri kipi kifanyike kuyaondoa haya yanayo chafua nchi yetu.
Natoa 'love' mbili mfululizo kwa andiko la mkuu 1000 digits'.