Jeshi la polisi, watafanyaje ili warudishe heshima na hadhi yao kwa wananchi?

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
1,222
Reaction score
2,912
Hakuna kitu kibaya katika utumishi wa umma kama kupoteza "trust" kwa watu unaowahudumia. Hili ni jambo linaloumiza na wakati mwingine kumpunguzia muhusika "confidence"

Jeshi la polisi limechafuka, limepoteza mvuto na hadhi yake imeshuka sana mbele ya wananchi. Hali hii ilianza muda mrefu sana lakini imekolea zaidi baada ya hizi heka heka za utekaji, utesaji, kamatakamata zisizo na mpango, matamko ya kejeli na kebehi kutoka kwa viongozi kwenda kwa wananchi na limehitimishwa na mauaji yaliyoratibiwa na jeshi hilo kipindi hiki

Hakuna namna yoyote sasa hivi mtu mwenye akili timamu atajivunia kuwa Baba au Mama yake ni polisi, kaka, mjombo, dada wala shangazi! Hawana siha nzuri mbele ya wanafamilia wenzao wenye akili timamu. Wananuka damu za watu! Mishahara na posho zao zinatoa harufu ya damu za watu!!

Kila aina ya maombi mabaya na laana vinaelekezwa kwao. Wamekosa mtetezi duniani na mbinguni! Hata sijui wakiona video zinazosambaa mitandaoni wananchi wakiwashangilia JWTZ wanjisikiaje? Hawaoni wivu?

Kabla mambo hayajaharibika sana, bado wanayo nafasi ya kujisahihisha hasa wakianzia kwenye kauli za viongozi wao. Wasijihisi kuwa wao labda ni daraja la juu kwani maisha yao tunayajua?

Siku nyingine nitawasema walimu, wanajua walichokifanya na nafsi zao zitawasuta hadi wanaingia kaburini
 
That ship has gone, labda kizwliwe kizazi kingone
 
Hao wanajulikana siku zote
ila jwtz ndo mshangao
watekaji tushawajua ni TISS
 
Lini walishawahi kuwa na heshima kwani mpaka wahofie kuipoteza ama kuirudisha.

Walichofanya ni uhalisia wao.

Polisi walikuwa wanaibia raia wakiwakamata na wakiona wanajeshi wanakimbia.
 
Screenshot_20251104-121708.png
 
Back
Top Bottom