Maadhimisho hayo yalikuwa yafanyike leo Jumatatu, Agosti 12, 2024, lakini Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Awadh Juma Haji lilitangaza kuyasitisha baada ya kutilia shaka tukio hilo akieleza kutokuwa rafiki kwa mustakabali wa nchi.
Soma Pia: Jeshi la Polisi lapiga marufuku mkutano wa BAVICHA siku ya vijana duniani
Polisi ilitangaza uamuzi huo ukitanguliwa na barua ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenda Chadema ya Agosti 8, 2024 kukitaka kusitisha shughuli hiyo, kwani lugha za viongozi wa Bavicha zinahatarisha usalama na zinakiuka sheria.
Mwananchi imefika eneo la Uwanja wa Ruanda Nzovwe na kushuhudia idadi kubwa ya polisi wakiwa na bunduki pamoja na gari la washawasha, huku wakiwa wamezunguka kona zote za uwanja huo.