SI KWELI Jeshi la Rwanda lathibitisha Paul Kagame kuwa kwenye hali mbaya ya kiafya

SI KWELI Jeshi la Rwanda lathibitisha Paul Kagame kuwa kwenye hali mbaya ya kiafya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu,

1750754045372.jpeg
 
Tunachokijua
Paul Kagame ni Rais wa Rwanda kuanzia mwaka 2000, awali Kagame amewahi pia kuwa mwanajeshi. Hivi karibuni zimezuka taarifa mbalimbali zinazouliza ni wapi alipo Rais Kagame na vipi pia kuhusu afya yake

Madai

Kumekuwepo na barua inayosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikionesha kuchapishwa June 23, 2025 yenye nembo ya jeshi la Rwanda ikieleza kuwa ni tangazo maalum kuhusu afya ya Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Uhalisia wa taarifa hiyo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa barua hiyo si ya kweli kwani haijatolewa na jeshi la Rwanda kama inavyoonekana.

JamiiCheck imefuatilia katika kurasa rasmi za jeshi hilo na kubaini kuwa barua hiyo haikutolewa wala kuchapishwa na wao kama inavyodaiwa. Aidha Barua inayosambazwa haina muhuri, haina jina la aliyeitoa wala sahihi yake.

Hakuna taarifa rasmi hadi sasa inayoonesha ni wapi alipo Rais Kagame wala hali yake ya kiafya, vilevile Jeshi la Rwanda kupitia ukurasa wake rasmi wa X limekanusha kuhusika na barua hiyo.

Kwa mara ya mwisho ukurasa rasmi wa X wa serikali ya Rwanda ulichapisha taarifa inayomuonesha Rais Kagame Mei 19 akiwa amehudhuria Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Usalama kuhusu Afrika (ISCA) uliofanyika Mei 19 na 20.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa;

“Zaidi ya wajumbe 600 kutoka nchi 70 wanahudhuria Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Usalama kuhusu Afrika (ISCA), ambao ni mkutano wa siku mbili unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kigali. Majadiliano katika mkutano huo yatajikita kwenye masuala mbalimbali yanayohusu changamoto na fursa za usalama barani Afrika.”
Ina maana poti mwenzangu GENTAMICINE Alidanganywa na informer wake!!?

Hypothesis:-

Dp world!!Kwa bandari za nchi pendwa!!

Na kama yule nabii wa Arusha utabiri wake wa mabaka mabaka wa Rwanda kukinukisha nchi pendwa utatimia nadhani chanzo ndio hiyo Bandari pale Brother atakapoanza KAZI ya kutindua usaha na kusitisha Yale malori tokea kule yanayobeba bidhaa hapo nchi pendwa bandarini!!

Na type kwa adabu aiseh!! sequence and series' imeanza!!

Nawaza!!hebu jaribu ku ignore huu utumbo nilioandika Mimi mlipa kodi!
 
una mengi sana lakini hata hiki ulicho'share' hapa si haba.
 
Back
Top Bottom