Troll JF
Platinum Member
- Feb 6, 2015
- 10,592
- 15,404
Makubaliano hayo yatajikita katika,
Kukabiliana na majanga na kutoa msaada wa kibinadamu ni sehemu muhimu ya kudumisha usalama wa kitaifa na wa kimataifa. Leo, Ubalozi wa Marekani uliwasilisha mahema tisa ya dharura kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania ili kuimarisha uwezo wa Tanzania wa kukabiliana na majanga. Mahema haya yatawawezesha wahudumu wa huduma za kwanza kuyafikia na kujipanga kwa haraka katika maeneo yenye dharura kuwahudumia watu walioathiriwa na moto au majanga mengine ya asili.
Makabidhiano haya yanaenda sambamba na kuzinduliwa kwa Programu ya Ushirikiano wa Vikosi vya Ulinzi wa Taifa vya Majimbo (State Partnership Program) kati ya Tanzania na Kikosi cha Ulinzi wa Taifa cha Jimbo la Nebraska (Nebraska National Guard). Katika nafasi yake kama Kiongozi Mkuu (Adjutant General) wa Nebraska National Guard, Meja Jenerali Strong pia ni Mkurugenzi wa Wakala wa Usimamizi wa Huduma za Dharura wa Nebraska.
Soma Pia:Tanzania na Marekani wakaribia kukamilisha makubaliano makubwa ya uwekezaji
Programu ya Ushirikiano wa Vikosi vya Ulinzi wa Taifa vya Majimbo unatoa fursa za kupanua ushirikiano ili kuimarisha uwezo wa kukabiliana na dharura na majanga.
Vibaraka hawaamini kinachotokea