Jeshi la Tanzania tulifikirie upya baada ya kushidwa na M23

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Je tuna jeshi hapa au ? Lazima tujiulize inakuwaje jeshi letu limeshidwa kirahisi na M23. Je tuna uhakika gani kama kundi dogo kama M23 likiingia Tanzania jeshi letu liko tayari na uwezo wa kisasa wa kupambana nao. Tunajua ni wajenzi wazuri na miradi mpaka ya sehemu za starehe lakini Jeshi letu sio lile tena na tunatakiwa badala ya kujidanganya tujipange upya.
 
Jeshi letu sio lile tena na tunatakiwa badala ya kujidanganya tujipange upya.
Mkuu unalizungumzia Jeshi la lipi hilo ambalo halipo kama sasa?

Ushauri wako ni mzuri, ila mifano yako bado sio valid kwenye hoja yako.
 
Watanzania hawana furaha kabisa na jinsi mambo yanavyoendeshwa kwenye nchi yao kila sehemu kujazwa uvccm sijui hata kama siku hizi wanaliombea jeshi lao ushindi vitani.
 
Sio kushindwa tu bali ni kushindwa kwa aibu kubwa mgambo qnakusainisha pepa of withdraw option.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Walienda na vifaa vya kijeshi na bunduki lakini wamerudi na bila chochote kile.vifaa n bunduki zao watasubilia CHATO Tanzania.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Tuache sisi tupo busy tunafanya mazoezi ya kuvunja matofali kwa meno na kurusha mateke 9/12
 
Akili yako ndogo, jeshi letu halikwenda DRC kupigana bali kulinda amani kwenye SADC mission.
Siyo kweli kaka. Jeshi la SADC lilienda kupigana kumlinda member state mwenzake kama ilivyo kwa NATO wanavyofanya Kwa member state mwenzao. Hatukwenda kulinda amani Bali kuwatoa M23 na ndiyo sababu mkwara wa kwanza ilikuwa ni kupiga kunguru (M23). Inasikitisha kuwa tulipigwa kama watoto wadogo..

Lile jeshi la Nyerere na Mkapa siyo hili la sasa. Kwa kweli tumeiaibika mpaka basi. Wanyarwanda wanatamba kuwa jeshi letu ni la kike.
 
Akili yako ndogo, jeshi letu halikwenda DRC kupigana bali kulinda amani kwenye SADC mission.

Tusijidanganye kwanini hawajapeleka mgambo. Kulikuwa na vita Congo na tumeshidwa huo ndiyo ukweli na jeshi limepoteza wanajeshi wake.
 
Subiria No reform No election, uone kilichomtoa kanga manyoa.
 
Unda jeshi lako mkuu, inaonyesha ni mdau mzuri kwa propaganda kuliko kujivunza! Pitia mikataba ya ulinzi wa Amani harafu uje tena!
 
Jeshi limesheheni MAKADA wa CCM na UVCCM, unategemea weledi gani hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…