Jeshi la Uhamiaji mmepiga gwaride zuri, sijawahi kuwaza hawa jamaa ni Askari

Jeshi la Uhamiaji mmepiga gwaride zuri, sijawahi kuwaza hawa jamaa ni Askari

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Hii nchi ina siri kubwa kwenye mfumo wa Ulinzi, Watendaji wa Uhamiaji ukikutana nao huwezi sema ni jeshi, Naamini Mwalimu wakati anatengeneza mfumo wa nchi aliona mbali Sana. Jinsi miaka inavyozidi kwenda ndipo Watanzania wanatambua kauli ya kwamba wananchi wote ni Askari.

Kama Hawa hjamaa ni Askari na namna wanavyotoa huduma bila Amri basi intelligence ya nchi ni kubwa. Naamini wanaweza kuwa wakusanya Taarifa zetu nyingi mipakani na wakati tunaomba pasipoti. Nimejifunza jambo kubwa Sana kwenye sherehe hii lakini nitoe wito Kwa Amri Jeshi Mkuu, pamoja na hao wapiga paredi nimwombe aendelee kusimamia mfumo wa awali ambao hakukua na uaskari kwenye huduma zao na hivyo kufanya watu kukaa na kufanya KAZI nao Kwa Uhuru na kusaidia kujua maadui kutoka nje na kuwazuia wasiingie nchini na wakiwemo tudhidi kuwabana.

Nakupongeza Mhe. Rais kwa hatua hii kubwa lakini pls tusiache history ikawabeba hawa Uhamiaji wakawa na mfumo wa huduma wa kijeshi maana Sisi Raia hawa tunashughulika nao maeneo mengi na yasiyo ya kialifu Bali ya huduma.

Pasipoti hazitolewi kijeshi mtatutoa kamasi, wageni wasihudumiwe kijeshi mtawatisha, hata majirani wanaoishi kwetu tusiwawekee ujeahi Sana tutabutua mahusiano ya kidiplomasia baina yetu na vyombo vya nchi zinazotuzunguka.

Mmefanya vyema Sana Uhamiaji hongereni I Diplomasia kwenu ni msingi mkubwa Sana.
 
Kamati ya ulinzi na usalama yote Ina full Askari walioiva
 
.... lakini nitoe wito Kwa Amri Jeshi Mkuu, pamoja na hao wapiga paredi nimwombe aendelee kusimamia mfumo wa awali ambao hakukua na uaskari kwenye huduma zao na hivyo kufanya watu kukaa na kufanya KAZI nao Kwa Uhuru na kusaidia kujua maadui kutoka nje na kuwazuia wasiingie nchini na wakiwemo tudhidi kuwabana.

Nakupongeza Mhe. Rais kwa hatua hii kubwa lakini pls tusiache history ikawabeba hawa Uhamiaji wakawa na mfumo wa huduma wa kijeshi maana Sisi Raia hawa tunashughulika nao maeneo mengi na yasiyo ya kialifu Bali ya huduma.

Pasipoti hazitolewi kijeshi mtatutoa kamasi, wageni wasihudumiwe kijeshi mtawatisha, hata majirani wanaoishi kwetu tusiwawekee ujeahi Sana tutabutua mahusiano ya kidiplomasia baina yetu na vyombo vya nchi zinazotuzunguka.

Mmefanya vyema Sana Uhamiaji hongereni I Diplomasia kwenu ni msingi mkubwa Sana.
Si umplekee barua hii huko Magogoni, unajua yeye haishi dodoma, bali anaishi karibu na bahari kama asili yake. Usiandike barua kwa rais na kuiweka hapa.
 
Wamechukua vijana wa JKT kuwaajiri ndio walioingia humo kwenye paredi
Mbn wanaenda mafunzoni kama majeshi mengine,wengi wamepitia chuo cha magereza kiwira-mbeya tena huchanganywa na wengine kwa nini wasijue?
 
Back
Top Bottom