Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

Nimejikuta naumia kwa story Yako...🥱. Pole Sana dadaangu ila bado muda upo, 30yrs unaweza ukarekebisha makosa yako na ukasimama Tena. Piga Goti inua mikono juu mlilie Mungu akupe moyo wa kukubaliana na matokeo na asikupe moyo wa kukata tamaa. Mungu humuinua mtu from 0% to 100%. Acha kujilinganisha na marafiki zako itakukosesha mood wa ku focus kwenye Target zako... Pole Sana
 
Amen, nashukuru sana mkuu
 
Lakini si huwa wanaambiwa wasimwamini mtu yoyote.
 
Acha uboya hakuna kitu Kama hicho.

Huyo bint wamempunguza kiaina ili hizo nafasi wapewe wengine.

Kiutaratibu Kama wamempima kweli wakaona hayupo fit ilibidi wamuweke wazi ana Tatizo gani ili ajue Kama siku sijazo anaweza kuaapply Tena au vipi?

Kutokuwa fit Kuna maana nyingi,unaweza usiwe fit kwa Sasa kutokana na shughuli ambazo ulikuwa unafanya mwanzo so ingehitaji muda had mwili ugain strong.

Haikuwa na haja ya kumficha,Hapo Kuna namna ilitafutwa ya kuwapachika watu wao.

Jamaa yangu jeshini walimwambia Kabisa kwamba hayupo fit sababu maisha ya uraiani aliyokuwa anaishi kabla hajaenda yamemlegeza Sana so wakawapa program maalum ya mazoezi wao peke Yao ili wawe fit kabla ya kuanza program ya pamoja na walio fit.
 
Huyo Jamaa yako hakukwambia ukweli,
Jeshini ukitengwa Kwa kigezo cha kupewa program maalumu basi ujue kwamba kilaza Kwa kile wanachokuwa wanakifundisha,
Wao kule wanaita NANGA,
Kwa hyo jamaa yako na hao wenzake walikuwa MANANGA na sio kwamba walikuwa unfit
 
Rushwa Rushwa Rushwa ,Rushwa ni dhambi na ni laana , unaweza furahia tu ilikufanikisha jambo lako lakini ikianza kuku affect ndio inagundua Rushwa ni kosa kubwa sana
 
Systemic corruption nchi hii ni shida sana ,watu wanaingia kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kwa corruption ,imagine raia huko mtaani sijui hali ikoje
 
Pole sana dada ila mambo mengine usilazimishe huwez jua Mungu anakuepusha na kitu Gani inawezekana kweli unachangamoto ya kiafya hivyo pengine ungeendelea na kozi yangekukuta makubwa zaidi,
hospital nyingi za serikali linapokuja swala la kupima afya Huwa wanajijazia form tu hata bila kufanya vipimo pengine uhamiaji wapo sahihi kwenye upande wa majibu ya afya Yako ila ninachowalaumu kwann hayo mambo wasingeyafanya kwenye usahili kabla hawajawaita huko kwenye kozi?
 
Pole sana kwakweli.

Naielewa changamoto unayoipitia mbaya zaidi una mtoto anakutegemea.

Mungu akusimamie usikate tamaa.

Kuna hali unaipitia hasa ukianza kuangalia wenzio uliosoma nao hatua walizopiga na wewe ulipo huwa inaleta stress sana.

Usiangalie wenzio jiangalie wewe mana katika maisha hatufanani na kuna wengine ni kama vile changamoto zimewekwa kwa ajili yetu.

Sali pia kama unaweza kufunga funga kwa Imani yako huku ukitafakari njia nyingine yakufanya.Kama una akiba kidogo igeuze mtaji jaribu kufanya biashara ndogo ndogo kama urembo wa kike kwenye hostel za vyuo,nguo za ndani au kawaida biashara yoyote hata kupika vitafunwa huku ukiendelea kujitafuta.

Kila la kheri na Mungu akupe nguvu
 
Asante nashukuru sana kaka, kilichokuwa kinanipa shida siyo kukosa nafasi, Nilijitahidi kulipokea kama lilivyo kuwa sijakidhi vigezo ila kilichokuwa kinaniumiza kichwa ni naanzaje kutokea pale, kwa sababu nilishajiaminisha kuwa naenda kupata kazi... lakini namshukuru sana Mungu kwa ajili ya JF kiukweli nimepata faraja mno nawashukuru wote kwa faraja, maombi na best wishes na hata waliokejeli pia nawashukuru sana... Mungu atubariki na atutetee sote...
 
Kawaida si kule hawataki mtu alie na mtoto. Yani mtu anaetegemewa sjui. Hwenda nd sabab walikutema
 
Pole Sana, nafasi yako imeuzwa pale pale Tanga,mkuu wa kambi ya mafunzo ndio mchezo wake
 
Sasa uliachaje biashara na kukimbiliya ajira? Ina maana hukuwa na mood na iyo biashara. Sasa umepoteza vyote. Karibu kuongea na ndugu wakuchangie mtaji hata laki tano tu uanze upyaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…