Auz
JF-Expert Member
- Apr 6, 2016
- 13,539
- 11,419
Kuna nafasi tamisemi Kada ya afya na elimu, jaribu huko.Shahada ya kwanza, maabara ya sayansi, mnashughulika na nini hasa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna nafasi tamisemi Kada ya afya na elimu, jaribu huko.Shahada ya kwanza, maabara ya sayansi, mnashughulika na nini hasa?
Nimejikuta naumia kwa story Yako...🥱. Pole Sana dadaangu ila bado muda upo, 30yrs unaweza ukarekebisha makosa yako na ukasimama Tena. Piga Goti inua mikono juu mlilie Mungu akupe moyo wa kukubaliana na matokeo na asikupe moyo wa kukata tamaa. Mungu humuinua mtu from 0% to 100%. Acha kujilinganisha na marafiki zako itakukosesha mood wa ku focus kwenye Target zako... Pole SanaNawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi. Amin
Wakuu maisha yana mitihani mingi sana wakati mwingine inakatisha tamaa na moyo unashindwa kuendelea, mimi ni mwanachama wa muda mrefu wa huu mtandao wetu pendwa wa JF ila kwa jina tofauti na hili nimeona nitumie hii akaunti mpya ili niwe huru kuomba ushauri na msaada wowote ule utakaoweza kunisaidia ili kutoka kwenye hii hali ninayoipitia.
Mimi mhitimu wa shahada ya kwanza fani ya maabara za kisayansi miaka 7 iliyopita, umri wangu ni miaka 30 sasa na pia ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 6 ambaye namlea mwenyewe kwa kila kitu.
Baada ya kuhitimu masomo nilifanikiwa kupata kazi ya mkataba katika shirika mojawapo la kimataifa na kupangiwa mkoa mmojawapo uliopo nyanda za juu kusini kwa miaka 3.
Baada ya mkataba kuisha nilirejea nyumbani jijin Dar na kufanya kazi kwa kujitolea katika taasis ya utafiti yenye tawi lake hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwaka mmoja na baadae nikaitwa tena kwenye mradi mwingine wa utafiti mkoa ule ule niliokuwepo kikazi mara ya kwanza kwa mkataba wa miaka 2, bahati mbaya sana baada ya miezi 3 tangu nianze kazi kukatokea changamoto ule mradi ukasitishwa na serikali na wale wafadhili wakaamishia mradi nchi jirani ya Zambia hivyo nikawa sina kazi.
Wakati hayo yanatokea mtoto wangu nilikuwa nimeshamuanzisha shule, kwa sababu ule mkoa tayari nilishauzoea nikaona nijiajiri kwenye biashara ya nafaka na mafuta ya kupikia japo kwa shida shida kwa sababu sikua nimejipanga kimtaji wakati nikiendelea kutafuta kazi, namshukuru Mungu biashara ikawa inaenda vizuri inanisaidia kukidhi mahitaji ya msingi ya kila siku.
Sasa mwaka jana 2022 nikawa nimepata changamoto kidogo nilinunua magunia ya alizeti mwezi wa 6 na kuyatunza nikitegemea nikamue mwezi wa 11/12 na kuuza mafuta wakati bei zinakuwa zimechangamka kidogo lakin badala yake ikawa kinyume bei ya mafuta iliporomoka zaidi nikalazimika kuuza kwa hasara kwa sababu ya uhitaji wa fedha niliokuwa nao.
Hivyo kiasi kidogo cha pesa kilichopatikana nilikitumia kuongeza nguvu dukani, kulipa bili nyinginezo kama kodi ya nyumba ninapoishi, kodi ya fremu na ada ya mtoto shuleni.
Wakati nikiwa kwenye mawazo ya hasara na kuporomoka kwa mtaji kinyume na matarajio, zikatoka nafasi za kazi za jeshi la polisi na Uhamiaji,nikaenda kufanya vipimo hospitali ya serikali ya mkoa kama ilivyotakiwa kwenye vigezo vya muombaji nashukuru nikakuta nipo sawa nikaomba zote na bahati nzuri nikaitwa kwenye saili zote, hivyo ikanibidi nichote tena kiasi cha pesa dukani ili niweze kufika kwenye usaili.
Nashukuru baada ya mchakato mrefu nikafanikiwa kuitwa kwenye kozi chuo cha Uhamiaji Tanga, kwa kweli nilifurahi sana. Hivyo ndani ya muda mchache wa maandalizi tuliokuwa tumepewa nililazimika kuuza duka na vyombo vyote vya ndani nilivyokuwa navyo japo kwa hasara, nikamuhamishia mtoto nyumban kwa wazazi wangu.
Pesa iliyopatikana kiasi nikamtumia mtu aliyenisaidia kupata nafasi kama shukrani, nyingine nikamlipia mtoto wangu ada ya shule ya mwaka mzima, nikanunua chakula cha kutosha angalau miezi miwili nyumbani na kiasi kilichobaki nikakitumia kwa ajili ya manunuzi ya mahitaji ya kule chuoni, nauli na akiba.
Basi siku ikafika nikaripoti chuoni, wiki ya kwanza ukaguzi wa vyeti na manunuzi ya vifaa vya kozi kama godoro, neti, tranka n.k ukafanyika, tukaendelea na mazoezi ya kawaida kuweka mwili sawa, mwanzoni mwa wiki ya pili zoezi la vipimo likafanyika na baada ya wiki moja majibu yakatoka bahati mbaya sana jina langu likawa moja kati ya majina ya watu walioonekana hawapo fiti kuendelea na kozi kwa mujibu wa vipimo vyao japo hatukupewa nafasi kujua tatizo ni nini kwa yeyote baina yetu.
Hivyo tukatakiwa kuchukua mizigo yetu na kuondoka eneo la chuo.
Katika siku nilizohisi kukata tamaa ya maisha na kutamani kufa ni ile siku natoka nje ya geti la chuo, kwa sababu kitu kikubwa kilichonijia kichwani kwa wakati ule ni kuwa naanzaje maisha upya tayari nilishauvuruga mtaji wangu nikitegemea tayari naenda kupata kazi ya kudumu, umri wangu umeenda, nina wadogo zangu watatu ambao bado wanasoma wazazi wanapambana ambao ninapokuwa vizuri nilikuwa nasapoti hapa na pale, nina mtoto wangu anayenitegemea kwa asilimia 100% baba yake tulishapotezana tangu nikiwa mjamzito.
Sasa na mimi naenda kuwa mzigo kwa wazazi nyumbani. Wakati ilibidi niwe msaada kwao, naumia sana.
Ndugu zangu ni wiki tatu sasa tangu hayo yatokee lakin bado moyo wangu una uchungu mno, wanasema muda unaponya mbona mimi hauniponyi?
Nahisi kukata tamaa nikiwaangalia marafiki zangu niliosoma nao wengi tayari wana maisha yao mazuri, natamani kuendeleza biashara zangu za nafaka, lakin sina pa kuanzia nilishavuruga mtaji, nikiangalia hali ya maisha hapa nyumbani ni ngumu basi nazidi kuchanganyikiwa nashinda tuu ndani sitamani kuonana na mtu yeyote.
Ndugu zangu wa JF naamin huku kuna watu wenye busara, uzoefu na nafasi mbalimbali za kunisaidia kwa namna yoyote ile, nahitaji ushauri wenu, msaada wa namna gani naweza kupata mtaji au hata connection ya kupata kazi itakayonisaidia kupata mtaji na kusimama tena akili yangu imeganda.
Nitashukuru sana na Mungu awabariki.
Asante mkuu, nitakutafuta Boss wanguPole mamii na sijui kwann sahv hunitafuti
Amen, nashukuru sana mkuuNimejikuta naumia kwa story Yako...🥱. Pole Sana dadaangu ila bado muda upo, 30yrs unaweza ukarekebisha makosa yako na ukasimama Tena. Piga Goti inua mikono juu mlilie Mungu akupe moyo wa kukubaliana na matokeo na asikupe moyo wa kukata tamaa. Mungu humuinua mtu from 0% to 100%. Acha kujilinganisha na marafiki zako itakukosesha mood wa ku focus kwenye Target zako... Pole Sana
Lakini si huwa wanaambiwa wasimwamini mtu yoyote.Nadhani Hilo jambo lake la Siri ni kuwa na mtoto....
Aidama Pole yako sana.Hukujua kama upo vitani? Kwenye kozi,kila mtu anapambania kumaliza kozi.Na hata hivyo mwanzo wa kozi tu Kuna Askari wakongwe nao hujifanya wanapiga kozi na nyie Huku wakiwa wapo kwenye Uchunguzi mzito wa mambo mengi ....
Nadhani haya ndio yaliyomtokea Kwa kutokana na Ushimen kama usemavyo......
Acha uboya hakuna kitu Kama hicho.Washangundua hizi hospitali za serikali wanahngeka HIVYO ukipima Haina shida ,nawao wanawataalamu wao wanakuja kujiridhisha ,muda mwingine wanaweza hata kukuinamisha wakiona mlango umetanuka kidogo basi hufai kua pale hata Hawa mabint waachane Sana kuwaruhusu wapenzi zao kutesti testi kugusa gusa jambio
Huyo Jamaa yako hakukwambia ukweli,Acha uboya hakuna kitu Kama hicho.
Huyo bint wamempunguza kiaina ili hizo nafasi wapewe wengine.
Kiutaratibu Kama wamempima kweli wakaona hayupo fit ilibidi wamuweke wazi ana Tatizo gani ili ajue Kama siku sijazo anaweza kuaapply Tena au vipi?
Kutokuwa fit Kuna maana nyingi,unaweza usiwe fit kwa Sasa kutokana na shughuli ambazo ulikuwa unafanya mwanzo so ingehitaji muda had mwili ugain strong.
Haikuwa na haja ya kumficha,Hapo Kuna namna ilitafutwa ya kuwapachika watu wao.
Jamaa yangu jeshini walimwambia Kabisa kwamba hayupo fit sababu maisha ya uraiani aliyokuwa anaishi kabla hajaenda yamemlegeza Sana so wakawapa program maalum ya mazoezi wao peke Yao ili wawe fit kabla ya kuanza program ya pamoja na walio fit.
Asante nashukuru sana kaka, kilichokuwa kinanipa shida siyo kukosa nafasi, Nilijitahidi kulipokea kama lilivyo kuwa sijakidhi vigezo ila kilichokuwa kinaniumiza kichwa ni naanzaje kutokea pale, kwa sababu nilishajiaminisha kuwa naenda kupata kazi... lakini namshukuru sana Mungu kwa ajili ya JF kiukweli nimepata faraja mno nawashukuru wote kwa faraja, maombi na best wishes na hata waliokejeli pia nawashukuru sana... Mungu atubariki na atutetee sote...Pole sana dada ila mambo mengine usilazimishe huwez jua Mungu anakuepusha na kitu Gani inawezekana kweli unachangamoto ya kiafya hivyo pengine ungeendelea na kozi yangekukuta makubwa zaidi,
hospital nyingi za serikali linapokuja swala la kupima afya Huwa wanajijazia form tu hata bila kufanya vipimo pengine uhamiaji wapo sahihi kwenye upande wa majibu ya afya Yako ila ninachowalaumu kwann hayo mambo wasingeyafanya kwenye usahili kabla hawajawaita huko kwenye kozi?
Kawaida si kule hawataki mtu alie na mtoto. Yani mtu anaetegemewa sjui. Hwenda nd sabab walikutemaNawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi. Amin