Mwalimu Nyerere wakati anabadilisha jina la jeshi kutoka East Africa Rifles na kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, alisema kuwa jeshi hili ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Jukumu lake la msingi ni kuwalinda Watanzania na kuilinda katiba ya nchi.
Kwa nyakati kama hizi ambazo dhuluma dhidi ya wananchi zimetamalaki kila kona: wananchi wanatekwa na kuuawa au kupotezwa, rasilimali za nchi zinaporwa
Dhulma dhidi ya haki za wananchi imekuwa ndiyo utaratibu wa kawaida wa watawala, ufisadi uliopindukia, udikteta wa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Chaguzi zimebakia kuwa maagizo na utaratibu wa kubariki uovu wa demomradia, ni lazima, na ni muhimu kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kusimama na wananchi, na kuwalinda dhidi ya dhuluma wanazofanyiwa.
Kufanya hivyo ni busara, ni kazi takatifu na kuliishi kwa vitendo jina lao, "Jeshi la Wananchi wa Tanzania". Hili ni jeshi la wananchi, siyo jeshi la watawala, siyo jeshi la wahuni wanamtandao, wala siyo jeshi la CCM, bali jeshi la wananchi katika ujumla wao.
Wakati polisi wamegeuka kuwa chombo cha kudhulumu haki za wananchi, TISS imegeuzwa kuwa genge la utekaji na mauaji, mahakama imegeuka kuwa chomba cha kudhulumu haki za wananchi; Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni muhimu na ni wajibu liwalinde wananchi dhidi ya dhuluma hizi zote.
Jeshi letu lina watu wengi wenye hekima na upendo wa kweli, ndiyo maana hawanyanyuki na kumfyatulia mtu risasi, bali wanatoa kauli za kuonya na kushauri.
Onyo lao lipo wazi kuwa polisi na wake watekaji wasiwadhuru wananchi wanaoilia na kuipigania haki yao, wakiwadhuru, wao watasimama kwenye wajibu wao, ambao ni kuwalinda wananchi dhidi ya madhulumati.
Watanzania tusikubali kuingia kwenye uchafu ulioitwa uchaguzi. Wananchi tunataka uchaguzi wa kweli, na siyo uhuni unaoendelea kwa sasa.